
Usafiri huu muhimu na wa haraka zaidi unaweza kusafirisha watu na mizigo kutoka bara moja hadi jingine una siri nyingi zaidi ndani yake.
Ndege ni miongoni mwa usafiri salama sana lakini pia ndio usafiri wa hatari zaidi pindi inapotokea hitilafu ya kiufundi,hali ya hewa wakati ikiwa angani,kwanikuna kuwa na asilimia kubwa ya watu wote waliomo ndani kupoteza uhai wao.
Miongoni mwa matatizo hayo ni swala zima la kufeli kwa mifumo ya kiufundi hasa ya injini zake ambayo ndio chombo pekee kinachoifanya ndege kukaa angani,kutua au kuruka.
Pindi inapojitokeza hitilafu ya kiufundi itakayosabisha injini moja au zote uikiwa mbili au nne kulingana na ukubwa wa ndege yenyewe kuzima basi hapo tumaini la kusalimika huwa ni sawa na asilimia 0%

Injini za ndege ziko za aina na ukubwa tofauti na zinatengenezwa na makampuni mbalimbali kama Rolls Royce,General electric,Alliance na nyinginezo nyingi.
Ingini za ndege ziko za aina mbili yaani zile za awali ambazo mapanga yake ukaa kwa nje kama hizi za Bomberdier za kampuni ya huko Canada na zile za kisasa zaidi ambazo mapanga yake ukaa kwa ndani.
Injini hizi ambazo utengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu zaidi na kisasa uwa na uwezo wa kunyanyua ndege kubwa za mizigo na abiria zenye tani nyingi zaidi ukilinganisha na zile za mapanga nje.

Injini moja inaweza kugahrimu dola za kimarekani milioni 13.5 hadi 35 hivyo kwa ndege za injini mbili au nne gaharama itakuwa zaidi ya hapo yaai mara mbilia ua mara nne .
Mfano kutengeneza ndege ya Airbus 380 moja tu inagharimu zaidi ya dola milioni 376 ikiwa sawa na shilingi bilioni 8,272,000,000 (bilioni nane milioni mia mbilia sabini na mbili) taslim.
Injini za ndege uathiriwa utendaji wake kazi na mambo yafuatayo:-

Kuingia kwa Ndege(Birds) ktk injini husika pia ni tatizo kubwa kwa injini kuweza kufeli kufanya kazi na kuifanya kusimama kabisa hivyo kuleta matatizo kwa chombo,mizigo na watu waliomo humo.

Injini moja ya ndege huwa na matundu 16 hadi 20 (Nozzles or Valves) ya kuchomea mafuta,hii ufanya kwa baadhi ya injini kutumia mafuta mengi zaidi.

Usukaji wa injini za ndege ni miongoni mwa mambo yanayotumia teknolojia ya hali ya juu sana.
0 Comments "JE WAJUA SIRI ILIYOPO NDANI NA NJE YA INJINI ZA NDEGE! NI VITU GANI VIANAWEZA KUATHIRI UTENDAJI KAZI WAKE?"