Serikali ya Tanzania imesaini mkataba mpya wa kuanza kwa ujenzi wa reli kiwango cha kati(standard gauge) ambapo kwa awamu ya kwanza utaanza Dar es salaam hadi morogoro na tayari imeshateng shilingi bilioni 7.6 kwa kuanzia makampuni kama rahaco,trl yanahusika ktk mkataba huo,reli hii inakusudiwa kufika mwanza na kigoma na kufika nchi za jirani kama Rwanda,kenya itatumia zaidi ya trilioni moja (1) taslim.
Ikimalizika treni itaweza kusafiri kwa kasi ya kilometa 160 kwa saa hivyo sawa na kusafiri dar es salaam hadi norogoro kwa saa moja na robo tu,na kufika mwanza kwa saa saba na nusu tu kitu ambacho kwa treni ya zamani inatumia zaidi ya saa 36 kufika mwanza.
Bank ya Exim ya watu wa China itahusika kutoa pesa za ujenzi wa reli hiyo ambayo ni muhimu kwa uchumi wa taifa na itarahisisha sana ktk sekta ya uchukuzi na usafirishaji wa watu na bidhaa mbalimbali.
0 Comments "SERIKALI YASAINI MKATABA KUANZA UJENZI WA RELI KIWANGO CHA KATI"