UGONJWA WA KANSA WAUMIZA VICHWA MADAKTARI

Ugonjwa wa kansa  umeendelea kusumbua wataalam wa Afya ulimwenguni kote kwa kushindwa kupata kinga na tiba  yake maalum.

Hii inatokana na aina nyingi zaidi ya mia moja (100) za ugonjwa huu na kila moja a ikiwa na sababu zake za kutokea hivyo kuleta ugumu ktk tiba yake. Mpaka sasa ugojwa huu unaendele kuua mamilioni ya watu ulimwenguni kote.
Baadhi ya aina za ugojwa huu ni  kanza ya maziwa,mapafu,ngozi,figo,ini,Mifupa,utumbo mkubwa na mdogo,damu,koo,sehemu ya njia za siri n.k
Kansa uletwa kwa kukua kwa semi za mwili bila  kiwango maalum na hatimae kuua nyingine na kuleta aina mpya ya seli  zilizokufa na hatimae vidonda.
Baadhi ya mambo au ambavyo vinaweza kukusababishia ugonjwa wa kansa:-
(1)Kuzeeka au kuwa na umri mkubwa.

(2)Vyakula vya kuzalishwa kimaabara au kibailojia kama wanyama na mimea.
(3)Vyakula vya kiwandani kama soda,pombe na vinywaji vyenginevyo.
(4)Uvutaji wa sigara na ana vyingine za vilevi.
(5)Kuwa na mambukizi ya aina mabalimbali ya virusi vya magonjwa kama ukimwi.
(6)Kurithi kizazi chenye ugonjwa huu kutoka kwa wazi.(Genetics)
(7)Kuchomwa na miale ya jua kali kwa mda mrefu zaidi.
(8)Uzito ulikithiri(obersity).

(9)Ulaji mbaya na matumizi ya madawa hovyo.

Ugonjwa huu mpaka sasa unaweza kwa njia kuu tatu tu japo sio za uhakika mtu  kupona kabisa.
Kupigwa miale au mionzi maalum,kufanyiwa operesheni na kuondolewa sehemu iliyoathirika na kutumia vidonge maalum kutuliza.
Ugonjwa huu ni hatari sana kwani huweza kumfanya mtu  kuanza kuoza sehemu iliyoathirika na kuweka kidonda kikubwa kisichopona daima,hivyo yatupasa kujilinda kadri ya uwezo wetu hasa na mitindo ya maisha,uvutaji wa sigara,unywaji wa pombe Kali,kutokula sana vyakula vya viwandani ili kupunguza hatari ya kupata ugonjwa huu usio na tiba ya uhakika mpaka sasa.
Kansa,ukimwi,kifua kikuu,malaria uua mamilioni ya watu ulimwenguni kila mwaka.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UGONJWA WA KANSA WAUMIZA VICHWA MADAKTARI"

Back To Top