AFRIKA,ASIA LINI KUTAISHA KUDHALILISHWA NA MAREKANI,ULAYA?

Imekuwa kawaida sana kwa nchi za afrika na asia kusikia zikipangiwa mambo mengi na matafa ya ulaya na marekani,kuanzia huduma za afya,miundombinu,elimu,maji na kupewa misaada mbalimbali ili kupambambana na kupunguza umasikini uliokithiri kwa nchi na wananchi wake wanaishi humo.

Kwa kutumia misaada wanayotoa kwa nchi hizi zinazojiita masikini wanaweza kuendesha kwa mambo mengi sana ikiwemo kutunga sheria ambazo zinataka zitumike na dunia nzima kama ya kusambaza demokrasia,sheria ya ndoa za jinsia moja yaani ushoga na usagaji na kufanya uingereza kutishia kutokutoa misaada kwa nchi ambazo zitakuwa zinapinga sheria hii ya ushoga na usagaji.

Itakumbukwa pia nchi hizi zimeshapiga marufuku viongozi na watu mbalimbali duniani kutkwenda ktk nchi zao kwa kisa cha kubana mambo ya kidemokrasia,kenya ktk uchaguzi uliofika walipigwa marufuku viongozi wasiingie marekani na nchi za ulaya kwa kisa uchaguzi haukuwa huru na wa haki.

Viongozi kama omar alli bashir wa sudan,robert mugame wa zimbabwe wamekubwa na adhabu hizi,hivi karibuni kumekuwa na tangazo kutoka marekani likizitaka baadhi ya nchi zaidi ya saba raia wake hawatoruhusiwa kuingia marekani na wala kuhamia kwa njia yeyote ile kwa kisngizio cha swala la tishio la mgaidi na ugaidi,ikimbukwe mwezi september 11/2001 baada ya shambulio kiltuo cha biashara marekani na kuonekana osoma bin laden ndio muhusika wa shambulio hilo raisi wa marekani wakati huo george bush alitangaza sheria ya ugaidi na kutumika na mataifa mengi na aliekataa kusaini sheria hiyo alisakamwa kwa mengi ikiwemo vikwazo vya kiuchumi na kuzuiwa kwenda marekani.

Hali hii inasikitisha sana hasa kwa nchi za kiafrika ambazo ndio zinategemea sana misaada ya mabwana wakubwa hawa kwa asilimia 60%,zinzjikuta ktk wakati mgumu sana ktk kukataa au kupinga lolote kutoka nchi za magharibi kwa kuogopa kunyimwa misaada,kutengwa,kuvamiwa kijeshi.

Nchi za magharibi zimekuwa zikitumia silaha hii ya kiuchumi,kijamii na kuweka vikwazo kama njia ya kulazimisha na kutia adabu kwa nchi zote jeuri zinzojaribu kupinga sera zao kama zimbabwe,sudan,korea kaskazini.

SWALI LA KUJIULIZA HIVI WAAFRIKA TUMEKOSA NINI KTK NCHI ZETU KINACHOSABABISHA MATAIFA YETU YASIWE KAMA YAO AMBAYO KILA SIKU TUNATAMANI KWENDA KUTEMBEA NA KUISHI HUKO?

Ukisoma historiana vitabu mbalimbal utaambiwa kuwa afrika na ulaya zote zilikuwa sawa ktk maendeleo hadi kufikia karne ya 21 na baada ya hapo ndipo tulipoanza kuachwa nyuma na wao,nzuri zaidi bara la afrika ndilo linasemekana kuwa bara tajiri na lenye kila rasilimali zinzohitajika kwa maisha na maendeleo ya mwanadamu ikiwemo madini,misitu,wanyama,bahari,maziwa,mito,ardhi yenye rutuba,mvua za kutosha na ndio maana wao wa magharibi walitamani na kuja kuzitawala nchi zetu na kubeba utajiri mwingi kupeleka kwao ulaya na kuapatengeneza na sasa sisi tunapatamani na kuhusi kama peponi.
Wapi tunakosea waafrika ktk kujenga na kupamba miji yetu au malighafi ipi inakosekana ikasababisha kutoweza kujenga barabara bora,nyingi na zuri,shule,vyuo,najengo ya serikali,ofisi,nyumba za kuishi,madaraja,kuweka umeme wa uhakika,hospitali na vifaa vya kisasa,ramani nzuri za miji,kuweka miji ktk hali nzuri kama bustani na vifaa vya takataka?

Tatizo ni pesa,wasimamizi,serikali,mafundi,elimu,rasilimali au watendaji? Hivi mpaka lini afrika tutaendelea kubuluzwa na kudhalilika kwa kupiga magoti na kuomba hata mambo yalio ndani ya uwezo wa mtu binafsi yanayohitaji utashi,ni mara ngapi tunapewa pesa na misaada ya vifaa,miradi mbalimbli na tukaona vifaa hivyo vikiishia kufanya kazi kwa muda mfupi sana na kufa ua kuharibika na kubaki historia?
Waafrika tuamke sasa mda wa kukaa na kusubiri misaada kwa asilimia 100% umekwisha,misaada ni utumwa mkubwa,unaekupa msaada kwa kila kitu kaa ukijua siku akihitaji lolote toka kwako huna budi kukubali.tuangalie nchi kama china,japan,india brazili na afrika kusini zote zilkuwa nchi masikini sana lakini leo mataifa hayo yanatuuzia vutu mbalimbali walivyotengeneza kwa mikono yao ikiweo gari,mitambo,nguo,bidhaa za nyumbani,pikipiki,simu(tata,toyota,howo,zongtong,yutong bu,,jiangfang,sanlg,toyo,boxer,simu kama tekno,itel,kompyuta kama dell,acer,tv singsung,ouling,aboder,mr uk,friji kama boss,subwoofer.

Ajabu ni kuwa hata marekani tunayiona leo ikipemndeza sana na kupendeza kiasi cha watu leo wanapigwa mkwala wasiingie nchi hiyo na waklalamika na kuandamana hovyo juu ya sheria hiyo wazungu wale walihamia kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo uingereza na kuanza kazi ya kuitengeneza nchi kwa juhudi,maarifa yao yote na hatimae sasa inaonekana sehemu ya ukweli ktk kila nyanja ya maendeleo,bara la marekani ya kusini lilikuwa pweke lenye watu wachache wahindi wekundu tu wakati christopher columbus anaingia pale mwaka 1492.

ajabu ya pili ni hii majengo na miundombimu iliyojengwa wakati wa ukoloni na utawala wa wajerumani na waingereza yanaonekana kuwa bora na imara mpaka sasa kuliko haya yanayojengwwa wakati huu wa uhuru(mungu atubariki na atuzindue waafrika)

Wapi tunakosea waafrika tujirekebishe tuwe kama wenzetu hawa?
 Tutoe elimu zenye maarifa na ujuzi wa fani na sio historia ya elimu,tuwe na uzalendo ktk mambo yetu binafsi ili tuwe  na taifa la wasimamizi waadilifu,tuachane na rushwa,sheria kali na gumu kwa wahujumu maendeleo,kufanya kazi kweli,kufanya mambo yanayolenga miaka 200 mbele na si mitano,
vyenginevyo tutendelea kunyanyasika mpaka mwisho wa dunia endapo tutakaa na kuendelea kushindana kisiasa,kupigana vita vya wenyewe,kukimbia elimu,kuhujumu mali za nchi na kupeleka magharibi,kuwa vibaraka wa nchi za magharibi.

Hii ni baadhi ya miji ya marekani na ulaya kama new york,paris,roma,washington dc,london na moscow.










Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "AFRIKA,ASIA LINI KUTAISHA KUDHALILISHWA NA MAREKANI,ULAYA?"

Back To Top