YAJUE MABWAWA MAKUBWA YA KUZALISHA NGUVU (NISHATI) ZA UMEME DUNIANI

Kwa sasa Tanzania inazalisha nguvu za umeme zipatazo  1,428 Megawatts ikiwa 1,358 ziko tkt gridi ya taifa na 70 megawatts zinajitegemea ktk mikoa mbali mbali.Umeme wa nchi hii kwa miaka mingi ulikuwa ukitegemea kuzalishwa kutokana na maji na mafuta mazito,ugunduzi wa rasilimali gesi wa maika ya hivi karibuni umeifnywa nchi hii kuongeza tena nusu ya umme ulikuwa ukizalishwa mwanzo.

Mikoa ya lindi na mtwara imekuwa ikitumia umeme unozalihswa na gesgi kutoka kisiwa cha songosongo na eneo la mnazi bay toka 2010,licha ya ugunduzi huu wa nishati ya gesi na mafuta ktk maeneo mbalimbali hasa mikoa ya kusini bado hali ya umeme nchini ni ,mbaya kutokana na kutotosheleza mahitaji ya nchi nzima,sababu zingine zinazosababisha umeme kusumbua ni miundomu chakavu,bajeti ndogo isiyojitosheleza ktk uendeshaji.

Licha ya iddadi ya watu kuendelea kukua usiku na mchana hadi sasa kufikia milioni 51 ni asilimia 15% tu ya watanzania ndio wanatumia nishati hii adimu ya umeme,asilimia 3% ya watu wanaoishi vijijini ndio wanatumia umeme na 97% hawatumii,asilimia 85% ya watanzania wote hawatumii umeme kabisa.

Umeme umekuwa chachu kubwa ya maendeleo toka kugunduliwa kwake ktk karne ya 18C,nchi nyingi za ualaya,marekani ya kusini na kaskazini,asia zimekuwa zikihangaika kwa nguvu zote ktk kuzalisha nishati hii kwa kutumia maji,gesi,mafuta,nguvu za jua,nyuklia n.k kwakuwa wanajua wazi kuwa viwanda na mambo mengi yanategea sana uwepo wa umeme wa kutosha.





Kutokuwepo kwa umeme wa uhakika ktk nchi ni tatizo kubwa sana ktk maenedleo ya mtu mmoja mmoja na hata kitaifa,barani afrika hali ya umeme ni mbaya sana isipokuwa kwa nchi kama Tunisia,Afrika kusini,Libya,Morocco,vyanzo vyote vya kuzalisha umeme tujaaliwa kuwa navyo ikiwemo maji,gesi,mafuta,uranium tatizo linabaki wataalam,uwezo wa kifedha na nia ya dhati kwa mamlaka husika.

Yafuatayo ndio mabwawa makubwa ya kuzalisha nguvu za umeme duniani:-

1.THREE GORGES  (china)

 Bwawa hili linapatikana nchi ya china ktk jimbo la Hubei,mchakato wa kujenga bwawa hili ulitiwa saini  1992 ila ujenzi wake ulianza 1994,gharama za ujenzi bwawa hili hadi kukamilka kwake wmwaka 2008 zilikuwa ni Yuan 180 sawa na dola za kimarekani bilioni 27.6$.

Urefu wa zaidi ya kilimita 1.12km ikiwa limefungwa genereta 32 za kuzalisha umeme zinazozalisha megawatts elfu 22,500 ikiwa ni mara 17 ya umeme wote unaozalishwa nchini Tanzania.

Ujenzi wa bwawa hili kubwa kabisa duniani ulichukua miaka 17 hadi kukamilika kwakwe rasmi mwaka 2008. Bwawa hili linapatikana ktk mto wa tatu  kwa urefu duniani YANGTSE

2.ITAIPU DAM (Brazil,Paraguay)

Ujenzi wa bwawa hili la pili kwa ukubwa  duniani ulianza rasmi mwaka 1971 licha ya mkataba wa makubaliano kutiwa saini mwaka 1966,bwawa linapatikana ktk mto Parana unaopatikana katikati ya nchi ya Brazil na Paraguay.

Gharama za ujenzi ni do;a bilioni 19.6$ za kimarekani,bwawa linazalisha megawatts elfu 14,000 MGW,ujenzi ulichukua miaka 18 hadi kukamilika,zaidi ya genereta 18 za kuzalisha umeme na ujenzi wa bawawa hili ulichukua takribani miaka 18 hadi kukamilika kwake mwaka 2003.

Mabwawa mengine makubwa duniani ni kama:-

3.XILOUDU (China 2014) 13,860 Megawatts





4.GURI (Venezuela 1978-1986) 10,275 Megawatts

5.TUCURUI (Brazil 1984) 8,370 Megawatts

6.GRAND COULEE (USA1942-1985) 6,809 Megawatts

7.XIANGJIABA (China 2014) 6,448 Megawatts

8.LONGTAN DAM (China 2009) 6,426 Megawatts

9.SAYANO-SHUSHENSKAYA (Russia 1989) 6,400 Megawatt

10.KRASNOYARSK (Russia 1972) 6,000 Megawatts

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "YAJUE MABWAWA MAKUBWA YA KUZALISHA NGUVU (NISHATI) ZA UMEME DUNIANI"

Back To Top