IJUE MELI KUBWA ZAIDI YA STEREHE DUNIANI

HARMONY OF THE SEAS ndio meli kubwa zaidi ya abiria duniani kuliko meli zote zilizowahi kuwepo huko nyuma,Meli hii imeanza kuundwa 2012 na kumalizika 2015 na kuanza shughuli zake rasmi 2016.

Meli hii iliyoundwa na kamp[un ya STX ya nchini ufaransa,wamiliki wa meli hii ni walewale wanaotoka ktk kampuni kubwa ya ROYALCARIBBEAN INTERNATIONAL Meli kubwa kama ALLUREOF THE SEAS,OASIS OF THE SEAS.

Meli hii ya Harmony of the seas imekuja na kuipiku meli iliyokuwa inashikilia nafasi ya kwanza kwa ukubwa ya ALLURE OF THE SEAS,Meli hii ya Harmony of the seas ni meli kubwa  yenye uwezo wa kubeba watu wapatao 8,461 ikiwa uwezo wake kamili ni zaidi ya tani 257,566 NT pia zaidi ya wafanyakazi au wahudumu 2,300 kwa ajili ya kuhakikisha mambo ya usafi,vyakula,starehe,burudani na na uongozaji wa meli nzima unakwenda sawa.

Aina hizi a meli ni ule mwendelezo wa meli mama ya TITANIC iliyoundwa nchini uingereza,meli hii ilipata jali ya kugonga mwamba wa barafu ktk bahari ya atlantiki mwaka 1912 ambayo ilikuwa na ukubwa wa mita 269 sawa na viwanja viwili na nusu wakati hii ya harmony of the seas ikiwa na mita 360 sawa na viwanja vitatu na nusu vya mpira wa miguu.

Ndani ya meli hizi ambazo utengenezwa rasmi kwa ajili ya sterehe kwa watu wenye vipato vya juu kama wanamuziki,waigizaji wa filamu,wanamichezo,wanasiasa na wafanyabiashara maarufu,gharama za ujenzi wa meli hii ni zaidi ya bilioni 1.35 za kimarekani kwa mwaka 2015.

Baadhi ya meli kama Queen mary I na II pia ni miongoni mwa meli zinazofanya kazi hiyo ya kusafirisha watu,sehemu kuu ambamo meli hizi upitia zaidi ni ktk miji ya Istanbul,hawaii,honolulu,portmouth na bandari nyingi maarufu za marekani na ulaya.








Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "IJUE MELI KUBWA ZAIDI YA STEREHE DUNIANI "

Back To Top