KUTANA NA VYAKULA VYA GHARAMA ZAIDI DUNIANI

Kuna vyakula vya aina nyingi sana ktk dunia tunayoishi,lakini si vyakula vyote vinaliwa na kila mtu,hii inatokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiuchumi,gharama,upatikanaji wa chakula husika ktk eneo,mila na desturi za watu husika,itikadi za kidini,sera za tawala,uelewa wa jamii hiyo juu ya chakula hicho n.k

Watu upendelea zaidi kula vyakula vinavyopatikana kwa wingi na tena kwa gharama nafuu ktk eneo wanaloishi,kuna baadhi ya vyakula vi[napatikana baadhi ya maeneo fulani tu duniani na sio kila eneo,lakini pia vipo vyakula ambavyo utumia gharama ya juu zaidi uzalishaji na uandaaji wake hivyo kufanya watu wengi kushindwa kuzalisha au kununua vyakula vya aina hiyo.

Hali ya hewa,aian udongo,maji ni miongoni mwa vitu vya muhimu zaidi ktk kuzalisha vyakula vya aina nyingi duniani,sio kila eneo unaweza kulima,kufuga kila aina ya mmea au mnyama.

Hivi ni baadhi ya vyakula vya gharama za juu zaidi kuwahi kuwepo duniani,asilimia kubwa ya vyakula hivi uliwa na watu maarufu,matajiri kama wachezaji mpira,wanasiasa,wafanyabiashara wenye vipato vya juu,wakati mwingine vyakula hivi uliwa kwa matukio maalum tu.

Hivi ndivyo vyakula maarufu na vya gharama ya juu zaidi duniani,baadhi ya vyakula vina gharama kubwa kiasi fedha yake unaweza kujenga nyumba ya kawaida iliyokamilika au hata kununua gari nzuri ya kifahari.

1.VYAKULA VILIVYOZALISHWA KWA UMBILE MAALUM


Vyakula vya matunda ambazo zinazalishwa kwa umbile maalum kama la moyo,mnyama na k.n ni vyakula vinavonunuliwa kwa gharama kubwa sana



JIBINI (MOOSE CHEESE)

Jibini hii maalum ufikia gharama ya dola $1,074 ikiwa sawa na pesa ya kitanzania shilingi milioni mbili na laki nne taslim.










3.DRY-CURED IBERIAN HAM
Ni chakula kinachopendwa kuliwa na watu wa nchi ya uhispania,ugiriki,macedonia na latin amerika,chakula hiki ugharimu hdai dola $392 ikiwa sawa na shilingi laki nane na thamanini elfu za kitanzania kwa mlo mmoja.










4.JAPANESE WAGYU STEAKS

Nyama hii inayotokana na ng'ombe maalum wanaofugwa nchini Japan inapatikana kwa gharama kubwa ya dola $450 sawa na shilingi milioni moja za kitanzania kwa kilo moja tu.











5.AYAM CEMAN BLACK CHICKEN

Kuku huyu mwenye nyama ya rangi nyeusi upendwa na watu wengi kwakuwa ana radha ya kipekee,kuku hawa wanapatikana maeneo machache duniani na hii kufanya kuku hawa kuwa wana gharama kubwa kupata nyama zake,kilo moja ya nyama ya kuku huyu mweusi ugharimu dola $200 sawa na shilingi laki nne na nusu.


6.WHITE TRUFFLES

Zao hili la mizizi linalo shabihiana kabisa na zao la tangawizi uzalishwa kwa gharama kubwa na utumika  kama kiungo kwa vyakula mbalimbali,kilo moja ya zao hili ufikia hadi dola $2,100 sawa na shilingi milioni nne na laki saba kwa kilo moja tu.












7.SAFFRON

Ni aina ya maua ambayo utumika kama kiungo ktk vyakula mbalimbali  na kilo moja tu ya majani haya ya saffron ufikia hadi dola $1000 sawa na shilingi milioni mbili laki mbili na nusu.










8.SWALLOW NEST SOAP

Huu ni mchuzi maalum unaotakana na ndege hawa wanaopatikana nchini china,mongolia,mchuzi na nyama yake iliyotaarishwa kitaalam ugharimu zaidi ya dola  $3,000 sawa na shilingi milioni sita na laki saba na nusu kwa bakuli moja tu la mchuzi.













9.KOPI LUWAK COFEE

Aina hii ya kawaha ya kipekee inayozalishwa ktk nchi za Indonesia,India na Ufilipino upendwa sana duniani hasa na watu wanaopenda kunywa kinywaji hikicha kahawa au kuchanganywa na vyakula au vinywaji vyengine.

Kahawa hii ugharimu zaidi ya dola $1,200 kwa kilo moja tu sawa na shilingi milioni mbili na laki saba.












10.MATSUTAKE MASHROOMS

Uyoga huu unaozalishwa nchini japan kiasili unapatikana pia ktk nchi chache za bara asia,uyoga huu mweupe unauzwa kwa gharama ya dola $600 kwa kilo moja tu sawa na shilingi milioni moja laki tatu na nusu.














11.WHITE PEARL ALBINO CAVIAR

Aina hii ya chakula kinachotakana na mayai ya samaki aina ya Albino Sturgeon wanaopatikana zaidi ktk bahari Ya Capsian iliyopo nchi ya urusi,samaki huyu ufugwa kwa gharama kubwa kwa mda wa miaka 2 hadi pale atakapokomaa kufikia uzito wa tani mbili ili kuweza kuzalisha mayai haya matamu na hadimu ulimwenguni,kilo moja ya mayai ya samaki huyu ufikia kiasi cha dola 9,100 sawa na shilingi milioni ishirini laki nne na sabini na tano elfu (20,475,000) za kitanzania.Aina hii ya chakula ipo pia ktk mayai meusi.aina nyingine ya samaki wanaotoa mayai haya ni Beluga ossetra,sevurga,salmon,steelhead,trout,lumpfish,whitefish,carp.





























SALMON RAW SLICED,SMOKED FISH MEAT

Huyu ni samaki maarufu sana duniani anayepatikana ktk baadhi ya nchi tu,samaki huyu uzaliana na kukua vyema ktk maeneo ya makutano baina ya bahari na mto,samaki huyu uishi sehemu zote za maji chumvi na maji baridi,samki huyu ukaushwa kwa njia za kiasili kwa watu wa norway,scotland.

Kilo moja ya nyama ya samaki huyu inagharimu zaidi ya dola $93 sawa na shilingi laki mbili na elfu kumi za kitanzania.









Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KUTANA NA VYAKULA VYA GHARAMA ZAIDI DUNIANI"

Back To Top