JE WAJUA KUWA NCHI ZA BAHARI YA PASIFIKI NDIO ZA KWANZA KUONA MWAKA MPYA!

Kwa mzunguko na ukubwa wa dunia nchi zilizopo upande wa mashariki ndio za kwanza kuona jua kabla ya zile zilizopo magharibi,kusini au kaskazini,hii ni kutokana na umbile la duara la dunia na mzunguko wake wa kujizungusha ktk mhimili wake kutoka upende wa magharibi kuelekea mashariki na kuzifanya nchi hizi zote za upende huo kuanza kuwa za kwanza kuliona jua kabla ya zile za magharibi.

Dunia kwa kawaida ina mizunguko miwili ambayo yote utoa matokeo taofauti,mzunguko wa kwanza nim ule wa dunia kulizunguka jua kutoka mashariki kuelekea magharibi(Revolution) Mzunguko huo uleta athari za kupatika Majira ya mwaka ktk vipindi vikuu vinne vilivyo gawanyika ktk miezi minne kwa kila kipindi kimoja yaani Kiangazi (Summer),Masika(Spring),Baridi(Winter),Kipupwe (Amtumn).Mzunguko huu ambao utumia siku 366 kukamilisha mwaka kamili yaani miezi 12

Mzunguko wa pili ni ule wa dunia kujizungusha yenyewe ktk mhimili wake ambao utumia saa 24 yaani siku moja kutoka upande wa magharibi kuelekea mashariki,aina hii ya mzunguko wa dunia ndio usababisha kupatikana kwa usiku na mchana kwa dunia yetu,kwa kulingana na umbile la dunia nchi zilizo pande ya mashariki ndio uwa za kwanza kuona jua au siku kabla ya zile za magharibi mwa dunia.

Kwa mtindo huu nchi na visiwa vya bahari ya pasifiki kama Kiribati,Tonga,Australia,Newzeland,Fiji,samoa,Kiritimati,Japan,Korea kusini ndio nchi za kwanza kabisa kuona na kushangilia sherehe hizi za mwaka mpya kabla ya nchi nyingine yeyote duniani.

Mfano nchi ya Tanzania ambayo iko upande wa mashariki mwa bara afrika inatofautiana kwa zaidi ya saa tisa (9) na nchi za Australia na Newzeland hivyo wakati  nchi hizi zikishangilia mwaka mpya kwa majira ya kwao ambayo itakuwa saa sita usiku basi nchini Tanzania na Kenya itakuwa saa tisa mchana.

Na visiwa vya Samoa ya marekani na Baker island ndio sehemu za mwisho kabisa kuuona mwaka mpya ktk uso wa dunia,hii kwakuwa visiwa hivi upatikana magharibi zaidi mwa dunia kuliko sehemu nyingine yeyote ile.

Tambua kuwa duniani kuna kalenda nyingi za kuangalia mwaka mpya ikiwemo hii maarufu inayo fahamika zaidi yaani Gregorian calendar ambayo ilianza kuhesabiwa toka wakati wa uhai wa Yesu mwana wa Mariam aliyezaliwa ktk mji wa Bathelehem (Yerusalem) Mashariki ya kati. Kalenda hii sasa inatimiza miaka 2018 toka kuanza kuhesabiwa kwakwe.

Baadhi ya kalenda nyingine zikiwemo za kidini ni kama za Hijri,Soviet,Pax,China Buddha,Hindu na nyingenezo nyingi.

Kwa mujibu huu sio kila sehemu au watu duniani usheherekea siku hii ya mwaka mpya huu tuliouzoea kwani jamii nyingi zina tamaduni na mila mbalimbali ambazo zina nyakati zao maalum ktk kusheherekea mwaka mpya wao.







Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "JE WAJUA KUWA NCHI ZA BAHARI YA PASIFIKI NDIO ZA KWANZA KUONA MWAKA MPYA!"

Back To Top