
Kuna mcanga unaopatikana ndani ya na pembezoni mwa mwambao wa bahari wenyewe uwa na kiwango kikubwa cha chumvi hivyo kuufanya kuwa sio bora zaidi ktk ujenzi,uko mchanga uanopatikana ktk mito,maziwa,jangwani .
Kwasasa ktk dunia mchanga sasa umekuwa bidhaa adumu sana na inayohitajika kwa kutumia njia yeyote ile,biashara hii imekuwa ikikuwa siku hadi siku hasa ktk miji mikubwa duniani ambapo kiwango cha ujenzi wa majengo marefu uko kwa kasi ya hali yajuu.
Kingo za mito na pembezoni mwa bahari zimeharibiwa kwa kiasi kikubwa ktk dunia kutokana na uchimbaji huu wa mchnga.

Duabai,Qatar,Singapore na Indonesia ni miongoni mwa nchi zinazolaumiwsa kwa kuhusika na baishara hii ya michanga,Biashara hii kwasasa inayoonekana kuwa na faida kubwa sana imekuwa ikimilikiwa na makampuni makubwa yanayoongozwa na magenge yenye nguvu ya kimafia.
Sehemu kubwa ya mwambao ya bahari imeharibiwa kwa kiasi kikubwa sana na kusababisha uharibifu wa kimazingira,mmomonyoko wa udongo,maisha ya viumbe hai wanoishi ktk maji,kuharibika kwa maeneo ya kilimo.

Kitu kimoja cha msingi ktk dunia kinapoondoshwa au kupotezwa ktk eneo lake la asili uleta madahara makubwa kwa eneo na viumbe waishio sehemu hiyo.
Ujenzi wa madaraja,maghorofa na majengo mengineyo utumia badhaa hii adimu ya mchanga ambayo uchanganywa na Saruji.

0 Comments "BIASHARA YA MCHANGA YATISHIA UHAI WA VIUMBE DUNIANI"