RAIS MAGUFULI AZINDUA BARABARA YA LAMI KALIUA-KAZILAMBWA TABORA

Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli akiwa ktk ziara yake ya kawaida mkoani Tabora ktk wilaya ya Kaliua amezindua barabara yenye urefu wa kilomita 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutoka makao makuu ya wilaya kaliua hdi kazilambwa.

Ujenzi huo ulio gharimu serikali zaidi ya bilioni 61.7 ikiwa ni pesa za serikali bila kupata msaada kutoka sehemu yeyote ile.Rais pia amemwagiza waziri wa ujenzi Mh.Makame Mbalawa kutafuta wakandarasi ktk kipande cha lami cha kilomita 28 na maeneo mbali mbali ambayo bado yanapitika kwa vumbi au changalawe ktk barabara hiyo kufanyiwa kazi kwa siku 45 tu wapatikane wataalamu wa kutengeneza maeneo hayo.

Pia amewatadhaharisha wananchi juu ya kuvamia maeneo mbalimbali ya hifadhi za serikali hasa misitu na barabara na kujenga kwakuwa wakitegemewa kulipwa kuwa watakuwa  wanautafuta umasikini wa wazi kwa wao wenyewe na vizazi vyao baadae,kwani serikali haitovumilia kabisa,hifadhi ya barabara inakuwa na upana wa mita 22.5 pande zote mbili ikiwa ni eneo maalumu,watu hawaruhusiwi kujenga au kufanya shughuli yeyote ile ya uchumi ya mda mrefu.

Rais amesisitiza juu ya matumizi ya barabara kujitahidi kuzitunza zaidi kwa kutokubeba mizigo sana inayopindukia tani 56.
Amewaasa wananchi kutunza mazingira kwa kufuga na kulima kwa umakini huku wakitunza mazingirsa kwa nguvu zao zote na kuacha kukata mkaa hasa kwa miti kama mininga.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "RAIS MAGUFULI AZINDUA BARABARA YA LAMI KALIUA-KAZILAMBWA TABORA"

Back To Top