TAMBUA MAAJABU MACHACHE KABISA YA MTO AMAZON

Katika sayari yetu hii ya dunia ambayo ni ya tatu ktk mzunguko wa dunia kuna aina kuu mbili za maji,waani Maji baridi (fresh water) na Maji chumvi (Salt water),Zaidi ya asilimia 3% ya maji yote yaliyopo duniani ni maji Baridi wakati asilimia 97% ya maji ni maji chumvi.

Bahari kama Atlantiki,Pasifiki,India,Aktiki,na Ile bahari ya kusini ndio zina kiwango kikubwa cha maji chumvi kuliko sehemum nyingine licha ya kuwepo maziwa na chemchem za maji chumvi ktk mabara.

Mito ni sehemu kuu ya maji baridi,kwa kawaida maji ya mito nyakati zote yako ktk mwendo yaani yanatoka sehemu za milimani au nyanda za juu na kuelekea sehemu za mabondeni hatimaye kuingiza maji yake ktk mabwawa makubwa amabayo sisi tunayatambua kama Bahari na Maziwa.

Kuna mito mingi sana inayoapatikana sehemu mbalimbali ktk dunia,mito hii utaofautiana kwa vyanzo vyake,asili,ukubwa,uapana,urefu,kiwango cha maji kinachotiririsha,kina,aina za viumbe vinavyoishi  na hali ya hewa ya maeneo ipiayo mito hiyo.

Mto Nile,Amazon,Mississipi,Congo river,YangTse,Mekong river ndio mito mirefu zaidi duniani na inasafirisha kiwango kikubwa zaidi cha Maji kwa sekunde na hatimaye kwa mwaka,mito mingi inamwaga maji yake ktk bahari zaidi kuliko sehemu nyingine.

Mto Nile unaopatikana Barani afrika ndio mto mrefu zaidi duniani ukianzia Ziwa victoria afrika mashariki na hatimaye kuishia nchini Misri kaskazini mwa afrika ukiwa na urefu wa kilomita 6,853 km ukipitia nchi za Uganda,Ethiopia,Sudan na nyinginezo.

Leo nimechagua kukujulisha machache sana juu ya mto AMAZON ambao ni wa pili kwa urefu Duniani ukiwa na urefu wa kilomita 6,992 km ukiwa umeanzia ktk Milima ya Andes inayopatikana ktk Bara la Marekani ya Kusini,sehemu kubwa ya mto huu iko ktk nchi ya Brazil amabyo ndio kubwa zaidi barni humo.

Chanzo kikuu cha mto huu kinajulikana kama MUNTARO ktk milima ya Andes,lakini hata hivyo mto huu mrefu unapita ktk nchi za Venezuela,Bolivia,Colombia,Ecuador,Peru na hatimaye Brazili na kumwaga maji yake ktk bahari ya Atlantiki.

Mto huu moja ya faida yake kubwa unapita ktk miji mikubwa ya bara hilo la marekani ya kusini zaidi ya miji 13 mikubwa,watu wengi wa miji hii wanautumia mto huu ktk shughuli nnyingi ikiwemo kilimo,ufugaji,usafiri,viwandani,matumizi ya maji nyumbani,uvuvi na utalii ktk pori kubwa linalofahamika kama Amazon Jungle.

Zaidi ya asilimia 25% ya maji yote yanayoingia katika bahari zote yanatoka ktk mto huu mkubwa.

Mto Amazon ni wa pili kwa urefu duniani baada ya mto nile lakini ni wa kwanza ktk kusafirisha maji mengi zaidi ukifuatiwa na mto Congo na hatimaye Nile.

Una ukongwe au umri wa miaka milioni 200 toka kuwepo ktk sayari hii.

Mto amazoni unaingiza maji zaidi ya lita bilioni mia mbili na tisa kwa mwaka (209,000,000) ikiwa ni sawa na maji yanayoweza kutumika na jiji kubwa la Ney York la nchini mareakani kwa zaidi ya miaka tisa (9).kwani jiji hili linatumia lita bilioni 26.5 kwa mwaka.

Zaidi ya mito midogo midogo 1,100 kutoka ktk vyanzo tofauti vinatiririsha maji yake ktk mto mkuu Amazon.

Kwa wale wapenzi wa kuangalia filamu za aina mbalimbali ambazo zinaonyesha mazingira ya misitu basi nyingi ktk hizo zinarekaodiwa ktk msitu huu mkubwa ambamo ndani yake unakatiza mto Amazoni.

Zaidi ya aina 3,000 za samaki zinapatikana ktk mto huu,250 za wanyama kama nyani,mamba,10,000 za miti mikubwa,70,000 za mimea mbalimbali na aina 1,800 za ndege uishi na kupatikana ktk misitu ya Amazon.

Eneo hili la Amazon liko ktk hali ya hewa ya Kiikweta hivyo kufanya kuwa na mvua mfululizo ktk kipindi chote cha mwaka na jua ktk nyakati zote,misitu iliyofungana,mvuke mkali,viumbe kama sokwe,kima,mamba,mijusi,vipepeo,na wadudu wa aina nyingi zaidi upatikana ktk eneo hili kuwa lenye hekari za mraba laki tano (500,000).

Asilimia kubwa ya mimea na wanyama wengi upatikana zaidi ktk eneo hili kuliko eneo lolote duniani,hii inafanya wataalam wa mimea,wanyama na tiba za magonjwa kupiga kambi katikati ya misitu hii wakifanya tafiti mbalimbali za mambo ya kitaalam.

Baadhi ya jamii zimekuwa zikifanya maeneo kama haya kuwa ni sehemu ya ibada au kuabudu miungu yao kama ilivyo kwa dini za Kihindu barani asia ambao ufanya maombi yao ya hijja maalum ktk mto GANGES.

Sehemu kubwa ya mto huu mrefu inatumiwa kwa kusafirisha watu na mizigo kwakuwa iko vizuri tofauti na ukilinganisha na mito mingi afrika ambayo haiwezekani kufanyia shughuli hii ya usafirishaji kutokana kuwa maporomoko mengi.



Share :

Facebook Twitter Google+
1 Comment "TAMBUA MAAJABU MACHACHE KABISA YA MTO AMAZON"

Back To Top