PROPAGANDA (Vile unayosikia au kuona sivyo ilivyo au ndivyo sivyo)

Wengi wetu si wageni sana na neno au msamiati huu ambao uanapatikana ktk lugha ya kingereza! Neno au msamiati huu una maana pana na kubwa sana hasa ktk medani za siasa za dunia na maisha ya kawaida ya kijamii.
Maana halisi wa neno PROPAGANDA ni hali ya kulifanya jambo lolote la kweli kuwa si la kweli na uongo kuwa kweli ktk kumuaminisha au kushawishi mtu au kundi la watu kuamini hivyo msemaji anavyosema.
Kwa maana nyingine PROPAGANDA haina tofauti na UNAFIKI,FITINA,KUSENGENYA AU UMBEA.
Kazi hii ufanywa na watu wenye uwezo mkubwa wa kuweza kupanga maneno,matukio kwa umakini zaidi kiasi kumfanya mtu anayeambiwa kuamini taarifa anazopewa kuwa ni za kweli kabisa ikiwa tu hatofanya utafiti wake wa ziada ktk kujiridhisha na taarifa hizo.
Kupitia aina mbalimbali za mbinu zinazotumika ktk kutimiza lengo hilo watu ujikuta wakiwachukia wenzao,ndoa kuvunjika,urafiki kuharibika au kuingia ktk migogoro mizito ya kifamilia,kijamii,kikazi na hata ya kimataifa.
Kupitia matumizi halisi ya neno hili unaweza kujikuta unapenda au kuchukia mtu,kitu au eneo fulani ikiwa tu hautofanya uchunguzi ktk kujiridhisha na taarifa ulizonazo juu ya mtu,kitu au eneo fulani.
Vita zote zilizowahi kupiganwa duniani hata ile ya kwanza 1914-1918 na ya pili 1939-1945 na hizi tunazosikia na kushuhudia sasa duniani sio zote zina sababu za kweli ktk kuahalalisha vita hizo.
Chukulia mfano wa kiongozi kama Adolf Hitler aliyezaliwa 1889 na kupotea 1945 akiwa na umri wa miaka 56 aliye iongoza ujerumani mwaka 1933-1945 pale alipotea kusikojulikana hadi leo,Yeye anafahamika kuwa ni kiongozi dhalimu na mkandamizaji wa haki za kibinadamu kwa dunia nzima ya sasa,kwakuwa tumekuta vitabu na kufundishwa hivyo juu ya wasifu wa kiongozi huyu anayeshutumiwa kwa mabaya mengi yakiwemo mauaji ya wayahudi milioni 6,uvamizi wa kivita nchi za ulaya,kutengeneza silaha za maangamizi na utawala wa mabavu.
SWALI LANGU LA MSINGI (JE DUNIA INAVYOMUONA NA KUMTAMBUA ADOLF HITLER KWA UBAYA WAKE NDIVYO VIVYO HIVYO WAMUONAVYO WAJERUMANI WENYEWE?
Kwa mda mrefu sana Ujerumani imekuwa ikishikilia nafasi ya kwanza kwa kuwa nchi ya kwanza ktk uchumi mkubwa barani ulaya na hata kwa dunia pia iko ktk nafsi nzuri,licha ya kuambiwa kuwa uingereza,italia,ufaransa na ubeligiji ndio mataifa ya kwanza kuenedelea ktk uchumia wa viwanda na teknolojia ya juu ktk miaka 1750s hadi 1850s.
Unaposoma historia yao ya kufikia uchumi na maendeleo makubwa hayo bila shaka hautaacha kutaja mchango mkubwa wa Adolf Hitler kwa zaidi ya asilimia 70%,hitler aliweza kuiondoa ujerumani ktk umasikini uliopindukia,uvamizi wa mataifa ya nje,kuongeza silaha na nguvu za kijeshi,miundombinu ya barabara,afya,elimu n.k.
Hitler hakuwa mtu wa kubabaishwa na taifa lolote wakati wa utawala wake wote wa chama cha NAZI,hitler alijua wazi kinacho tusababisha kuwa masikini wa kutupwa sio ukosefu wa rasilimali au watu bali ni udhaifu wa kusimamia sera,sheria na kanuni ktk utekekelezaji wa mambo yao wanayoyapanga.
Ni muhimu sana kwa mwanadamu kufanyia utafiti au uchunguzi wa kina kwa kila taarifa uzosikia,kupewa au kuona kabla ya kutoa maamuzi au kukata shauri,hii itaepusha sana kuleta madhara yatokanayo na athari za Propaganda.
(Wenye mawazo chanya bila shaka watakuwa wamenielewa vyema)






Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "PROPAGANDA (Vile unayosikia au kuona sivyo ilivyo au ndivyo sivyo)"

Back To Top