NI VYEMA WASANII BONGO MOVIES TUKAJIFUNZA KUTOKA KWA WAIGIZAJI BARA ULAYA NA MAREKANI YA KASKAZINI

Nimekuwa mfutiliaji na mtazamaji mkubwa wa filamu za kutoka bara ulaya na marekani ya kaskazini hasa United states of Amerika hasa kuanzia mwanzoni mwa miaka 1990s hadi sasa,nyakati huo nina umri mdogo,kabla ya hapo soko la filamu za kihindi zilikuwa zikitamba zaidi kuliko nyingine zozote duniani ila ghafla hali hii ilikuja kubadilika kwa soko la filamu kutoka bara ulaya na marekani kuanza kuingizwa nchini.

Licha kipindi hiko sikuwa naelewa lugha yeyote iliyokuwa inatumiwa ktk filamu hizo za kihindi na kizungu yaani nikimaanisha kingereza na kihindi ila nilijikuta nikivutiwa sana na mapangilio wa matukio yaliyo ktk filamu hizo hasa kwa jinsi waigizaji wa filamu hizo walivyoweza kuzitendea haki nafasi zao za uigizaji ktk filamu hizo.

Sote tunakili kuwa kutoelewa lugha inayozungumzwa ndani ya kazi ya sanaa ni miongoni mwa kikwazo kikubwa kinachoweza kumfanya mtazamaji au msikilizaji wa igizo au nyimbo hiyo kutoitilia maanani au kutoitazama kabisa,lakini hii imekuwa tofauti sana kwa wenzetu wa bara ulaya wao wamekuwa makini sana ktk kuigiza kwao kwa kuhakikisha mtu anayeigiza ktk nafasi husika basi anafaa kwa kuanzia maneno,mwonekano,vitendo,mavazi na hata hali ya kimazingira.

Unapokuwa unatazama filamu za kutoka nje ya bara la afrika haitakuchukulia mda kujua nani ameigiza kama adui au mtetezi au starring kama tulivyozoea,hii inatokana na mwonekano wa msanii husika ktk kila jambo alifanyalo ndani ya filamu hiyo,upangiliaji mzuri wa mtiririko wa kisa kizima ndani ya filamu hiyo.

Watu hawa huwa wanadumu sana na wasifu wao ktk uigizaji wao karibu ktk kila filamu utakayomuona yeye mara zote atacheza ktk nafasi yake hiyo hiyo,hii imekuwa tofauti sana na hali ya uigizaji wa filamu za hapa nchini Tanzania au afrika mashariki kiujumla,wasanii wamekuwa wakijitamba kwa kuweza kufanya kila jambo ndani ya fani hii,yaani unaweza kukuta msanii ktk filamu moja yeye ndio muongozaji,mhariri,adui na kazi nyingine nyingi wakati ktk uhalisia kazi hizi zinatakiwa kufanywa na watu tofauti kabisa tena wenye utaalamu wa hali ya juu ktk idara hizo.

Waigizaji wengi wa filamu hapa nchini wamekuwa wakileta hisia binafsi wakiwa ktk kazi za uigizaji {location} yaani mtu anataka kuvaa mavazi yatakayomendeza yeyen binafsi badala ya hali halisia ya anayotaka kuigiza,kuongea maneno ya kwake,kujiweka mapambo au aina za mitindo ya nywele ambayo haendani kabisa na anachokiigiza kwa mda huo,kulazimisha kucheza nafasi ambayo hakidhi vigezo au kukataa kucheza nafasi fulani hata kama sura na matukio yake yanaonyesha kufaa kucheza hivyo.

Shida nyingine ktk fialmu za hapa nchini ni juu ya kufanya makosa ya wazi ktk kuhariri kazi hizo,filamu nyingi nilizowahi kutazama nimekuta makosa ya wazi ktk vitendo,maneno au mpangilio wa igizo husika ila ajabu zaidi nashangaa imekuwaje kwa filamu mpaka inafikaq sokoni hatimaye kwa hadhira bila kurekebishwa makosa hayo ya wazi kabisa wakati filamu  hiyo imepitia kwa wahariri na waongozaji ambao wanapaswa kuondoa makosa hayo toka nyakati za uigiazaji au kuhariri.

Baadhi ya filamu watu wa kamera ujikuta wakichukua matukio,maeneo au watu wasiohusika kabisa ktk filamu hiyo na wala hawana mchango wowote na kisa hiko kinachoigizwa,hali hii huwezi kuikuta sana kwa filamu za bara ulaya wala marekani kwani kia kinachoonekana ndani ya filamu hiyo basi kina mchango mkubwa ktk kuelewa kisa kizima.

Tatizo la kisa kizima cha filamu kuweza kujulikana na mtazamaji mapema au mwanzoni tu mwa filamu husika,hii inamfanya mtazamaji kukosa hamasa ya kuendelea kuatazama filamu hiyo,kurejea visa vyenye maudhui sawasawa na filamu nyingine tena mbaya zaidi kuigiza kwa mtindo uleule wa filamu iliyoigwa  copy nad paste,ni nyema wasanii kuwa wabunifu sana ktk kuunda na kubuni visa ktk filamu zao kwani wakati fulani mtazamaji anaweza kuitazama filamu mwanzo hadi mwisho kisha akashindwa kuielewa au kuonanisha matukio ndani ya igizo hilo,wakati mwingine filamu uanza na kuisha tofauti na kisa cha awali.

Nafahamu kuwa tuko nyuma ktk teknolojia ya vifaa,wataalamu na waigizaji nchini lakini sifikiri kama kwetu itatuwia vigumu zaidi ktk kufanya vyema kwkuwa sisi kazi yetu ni kununua tu vifaa vizuri vya kazi zetu tofauti na wenztu ambao wao ilibidi wakae chini na kuumiza akili ktk kutatua changamoto hizo hadi wakafanikiwa.

Wasanii wa nchini wamekuwa wakilalamika juu ya watu kutokuwa na uzalendo na kazi za nyumbani na kukumbatia kazi za nje zaidi,hali hii inatokana na makosa yetu wenyewe kwa kutoa filamu zisizo na viwango wala kuhamasisha mtu kutazama maigizo hayo.



Hongera sana kwa marehemu Steven Kanumba hasa ktk filamu yake ya Devils Kingdom na nyingine nyingi kwa kuzitendea haki kwa kiwango kikubwa kiasi cha kumfanya mtu kuweza kukaa chini na kuatazama mwanzo hadi mwisho bila ya kuwa na makosa ya sauti ya kuapnda na kushuka,video chafu au mapngilio mbovu wa matukio.

Wako wasnii kama Mzee Magari,Jengua,Msisiri,Muhogo Mchungu,Bi mwenda,Madebe Lidai,Cloud 112,JB na wengine wengi nambao wengin wao tulishazoea kuwaona ktk maigizo ya miaka ya nyuma na ndio hao hao leo wanauvaa uhalisia wao vyema ktk fialmu za sasa.

Natambua kuwa kuna changamoto za pesa mitaji,mazingira ya kufanyia kuigiza,watu wenye utaalam wa kusimamia zoezi zima la uigizaji lakini ni vyema zaidi ikiwa kila fialamu inayoigizwa basi ikatendewa haki kwa uamkini zaidi ikiwezekana kwa mda mrefu ilili inapotoka iwe kazi yenye kupendeza na kusisimua hadhira na kuendana na maisha halisia ya jamii husika.

Wenzetu wamekuwa wakitumia mda na gharama nyingi sana ktk kuigiza filamu moja tu lakini pindi inapotoka ukweli urudisha gharama zote kwa watu kuzipapatikia sokoni,si aiabu filamu moja ikatumia mailioni ya dola na kuigizwa zaidi ya miaka miwili au mitatu tena ktk nchi tofauti tofauti duniani ili kupata uhalisia wa wa filamu hiyo na kukamata nyoyo za  hadhira.

Tuwe na utaratibu wa kutazama kazi za nje kwani zinaweza kutupa ujuzi na uzoefu mkubwa sana ktk kuigiza filamu zetu zijazo.

Nimamua kutumia picha za waigizaji wawili maarufu CARY-HIROYUKI TAGAWA mwenye asili ya kijapani na alieyuvuma zaidi ktk filamu ya Showdown little tokyo ya mwaka 1991 iliyoigizwa na Dolfph Lundgren  na Brandon Lee,Tagawa yeye aliigiza mhalifu mwenye kundi kubwa la kimafia ambalo lilikuwa likiendehs shughuli zake za kihalifu,ubakaji na unyayasaji,wizi ktk mitaa ya jiji Tokyo Japan,Tagawa alizaliwa Japan Septemba 27 1950 kwasasa ana umri wa miaka 67na ana uraia wa Marekani pia na Urusi.

Pia nimetumia picha ya Amrishlal Puri raia wa India marufu kwenye filamu za kihindi akiwa anaigiza kama mhalifu au adui mwenye kumiliki magenge ya vikundi vya kihuni,Amrishlal Puri alizaliwa Juni 22 1932 jimbo la Punjab india.

Muigizaji huyu nguli wa filamu za kihindi aliyekuwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 20$ aliyefariki Januari 12 2005 ktk jiji la Mumbai {Bombay} nchini India.

















Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "NI VYEMA WASANII BONGO MOVIES TUKAJIFUNZA KUTOKA KWA WAIGIZAJI BARA ULAYA NA MAREKANI YA KASKAZINI"

Back To Top