JE WAJUA KUWA JENGO LA IDARA YA ULINZI MAREKANI (PENTAGON) NDIO OFISI KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI!

Kuna mambo mbalimbali ambayo ushindanishwa kutokana na sifa mbalimbali zikiwemo ukubwa,uzuri,gharama,urefu,umaarufu na sifa nyinginezo,leo niko hapa kwa ajili yam kukujuza juu ya jengo ambalo toka kumalizika kwake kujengwa hadi leo bado linashikilia nafsi ya kwanza duniani kwa kuwa ndio jengo lenye ofisi nyingi zaidi ktk sehemu moja kuliko jengo lingine lolote hapa duniani.

Sehemu hii hatushindanishi urefu wala gharama za jengo hilo bali ni ukubwa wa eneo na wingi wa ofisi zake zinazoptaikana ndani ya jengo hilo moja tu,marekani kumekuwa na majengom mengi sana makubwa ,marefu,kifahari na ya gharama za hali ya juu sana,baadhi ya majengo haya yakiwemo hoteli,makazi,viwanda,viwanja vya michezo na hata maofisi,mfano wa majengo hayo ni kama lile la kituo cha biashara cha dunia WTC kilichoharibiwa na tukio la ugaidi septemba 11 2001,jengo hili lilikuwa na  ghorofa zipatazoi 110,white house,empire state building n.k

PENTAGON ndio jengo au ofisi kuu ya idara ya mambo ya ulinzi na usalama wa nchi ya marekani,ujenzi wa jengo hili ulianza rasmi septemba 11 1941 chini ya utawala wa rais wa awamu ya 32 wa marekani  Franklin D Roosevelt aliyoingoza marekani toka 1933 hadi alipofikwa na mauti april 12 1945,jengo hili lilijengwa usiku na mchana kwa mda wa miezi 16 tu na kufanya kukamilika 1943,zaidi ya tani 680,000 za mchanga na mawe kwakuwa sehemu kubwa ya jengo hili imejengwa kwa zege kali,zaidi ya dola milioni 83$ za kipindi hiko zilittumika kujenga jengo hilo.



Mji wa Arlington ktk jimbo la Virginia ambapo ndipo sehemu kubwa ya ofisi za idara ua ulinzi na usalama za marekani zimejengwa huko ikiwemo na kambi ya utafiti ya kijeshi inayojulikana kama Area 51 pia iko huko,zaidi ya hekari 34 zimetumika kujenga jengo hili,urefu wa kwenda juu wa jengo hili ni futi 77 kutoka chini,futi milioni 6.6 ujumla wa eneo lote.

Njia zote (Corridors) zilizomo ndani ya jengo hilo linasemekana kufikia zaidi ya kilomita 28 sawa na maili 17.5 za urefu wake,zaidi ya makampuni 70 ya ujenzi na wakandarasi wasipungua 1000 walihusishwa ktk kuchora ramani na kujenga jengo hilo kubwa la ofisi duniani,zaidi ya hekari 5 zimetumika kujenga maduka makubwa (Plaza) yanayosaidi wafanyakazi ndani ya jengo hilo ktk huduma mbalimbali.

Ofisi hii imengwa jirani kabisa na mto Potomac ili kurahisha ujenzi wake ktk huduma za matumizi ya maji kabla ya ujenzi na hata baada ya ujenzi huo kutumiwa ndani ya jengo hilo kubwa kabisa.

Zaidi ya wafanyakazi elfu  30,000 wameajiliwa ktk jengo hili wengi wao wakiwa ni wanajeshi na watu wa vitengo vya FBI,CIA,NSA na watu wengine wa usalama wapatao elfu 23,000,raia wapato 3,000 wakiwa kama wafanyakazi mbalimbali ndani ya jengo hili.

Ofisi za Mkuu wa idara ya usalama (Joint Chief Of Staff) ipo ndani ya jengo hili ambaye yeye pia upokea maelekezo toka kwa Waziri wa ulinzi ambayo bila shaka utoka kwa rais wa marekani.

Zaidi ya mikono ya simum ipatayo elfu 45,000 iko ndanin ya ofisi zilizopo ndani ya jengo hili,kwa mda wa saa 24 tu upokea simu zipatazo laki 280,000 kutoka ndani ya marekani na sehemu nyingine duniani.

Jengo hili lilijengwa kwa makusudio makubwa ya kujipanga vyema ktk kuhakikisha kushinda vita kuu ya pili ya dunia ambayo ilikuwa ikiendelea 1939-1945.

Idara ya ulinzi na usalama ya marekani ndio idara yenye waajiliwa wengi na inasemekana kutmia pesa nyingi sana ktk bajeti ya nchi hiyokwakluwa na mipango mingi ya kiulinzi ktk dunia nzima,ikumbukwe marekani ndio nchi yenye watu wake wa ulinzi karibu ktk eneo duniani pia wao ndio wana kambi za kijeshi ktk nchi mbalimbali kwa kusudio la usalama wa taifa na nchi marafiki zao. baadhi ya nchi ambazo marekani anavyo vituo vya kijeshi ni Japan,South korea hivyo kuifanya idara hii kutumia pesa nyingi ktk kuendesha vituo hivi,kulipa mishahara,vyakula,mafuta,utafiti,malazi na vifaa vya kijeshi.

Pentagon utumia asilimia 93% ya mafuta yote ya marekani zaidi ya galoni bilioni 4,600,000,000 za mafuta ya aina mbalimbali ya mitambo ya kijeshi utumika na idara hii hii ikiwa sawa na galoni 48,000,000 za mafuta kwa siku moja tu,pia utumia zaidi ya gigawatts elfu 30,000za umeme kwa mwaka ambazo ugharimu zaidi ya dola bilioni 2.2 za kimarekani.

Marekani utumia zaidi ya dola bilioni 1.6 kwa siku ktk kuendesha mambo yake na dola milioni 250 kwa siku kwa mambo ya kivita pekee huko afghanstan,iraq,syria n.k,zaidi ya dola bilioni 68 kwa ajili ya shughuli za kijeshi zinazoendeshwa kisiri ndani na nje ya marekani,hali hii uifanya marekani kutumia zaidi ya dola 1.46 kwa mwaka toka 2001.

Jeshi la ardhini Ground troop,Anga USAF,wanamaji Navy,DOD vyote ni vitengo vinavyohusika kuratibu shughuli zake zote ndani ya jengo hili kubwa kabisa na hii ndio maana ikalifanya jengo hili kuwa na ofisi nyingi zaidi kuliko jengo lolote duniani hadi sasa licha ya kuwa na umri wa miaka 75 toka kujengwa kwake.

Inasemekana jengo la The Abraj Al Bait ambalo liko ktk hatua za mwisho za ujenzi wake nchini Saudia arabia ktk mji wa Mecca litakapomalizaika mndio liatakarovunja rekodi kwa kuwa jengo kubwa la ofisi duniani hivyo kulishinda Pentagon.













Frankilin D Roosevelt rais wa 32 wa marekani aliyefanikisha ujenzi wa jengo la pentagoni ktk kipindi cha utawala wake.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "JE WAJUA KUWA JENGO LA IDARA YA ULINZI MAREKANI (PENTAGON) NDIO OFISI KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI! "

Back To Top