UHURU AU ODINGA KUJULIKANA JUMANNE IJAYO KENYA

Uchaguzi wa kenya ktk kumtafuta rais,wabunge,magavana na maseneta kufanyika jumanne ijayo tarehe 08/08/2017 baada ya miezi kadhaa ya purukushani za kampeni za uchaguzi kenya.

Wagombea uraisi kutoka


vya vya upinzani na chama tawala cha Jubilee wamejitokeza ktk kampeni hizo zilizodumu kwa mda mrefu zikiwa na malalamiko kwa rais Uhuru kenyatta kuhisi kuwa Tanzania inaweza kuhusika kufanya udanganyifu ktk matokeo ya baadae ya uchaguzi wa kwa kutka kumwingiza Raila odinga madarakani kwa kisa cha mgombea huyo wa upinzani kuonekana mara kadhaa kuwa karibu ssna na raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh.John Joseph Magufuli nchini Tanzania.

Wakenya zaidi ya milioni 19 wamejiandikisha na kukidhi vigezo vya kupiga kura ktk uchaguzi wa mwaka huu 2017.

Kenya imepata historia mbaya baada ya uchaguzi uliomwingiza Mh Mwai Kibaki madarakani ktk kipindi cha mwisho cha mwaka 2007 baada ya vyama vya upinzani kuhisi kubadilishwa kwa matokeo yalimtaja Mwai kibaki kuwa mshindi wa uchaguzi huo hivyo kuwalazimu wapinzaini kuingia barabarani kuingia barabarani na kuleta machafuko na mauaji ya kikabila.

Kenya kumekuwa na tatizo la ukabila ambalo linasumbua nchi hiyo kwa mda mrefu hassa kwa makabila ya wakamba,wakikuyu na wajaluo ambao kila kabila moja wapo linahitaji kushika ngazi za juu za serikali hiyo.

Kenya imekuwa ndio nchi yenye uchumi mkubwa ktk nchi za afrika mashariki na ndio ilikuwa mbali zaidi ktk maendeleo ya kiviwanda,ktk kilimo piakenya iko mbali ukilinaganisha na nchi nyinginezo.

Hivi karibuni serikali imezindua reli ya Standard gauge iliyojengwa kutoka mji wa nairobi hadi maombasa yenye urefu wa zaidi ya kilomita 400,reli hii inayofahamika kama MADARAKA inakusudiwa kuinua na kuimarisha zaidi shughuli za kibiashara na uchumi kijumla kwa kutoa mizigo toka bandari ya mombasa hadi mji wa nairobi.

Jumanne ijayo ndio siku rasmi kwa wakenya kufanya uchaguzi huo mkuu ambao uanaweza kumaondoa au kumrudisha madarakani Uhuru Kenyatta.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UHURU AU ODINGA KUJULIKANA JUMANNE IJAYO KENYA"

Back To Top