KINDUMBWENDUMBWE CHA UCHAGUZI RWANDA CHAFIKA UKINGONI LEO

Baada ya miezi kadhaa ya kampeni zilizokuwa na mbwembwe za ushindani kati ya chama tawala cha Rwandan Patriotic front (FPR)  na vyama kadhaa vya upinzani vilivyoweka waagombea kushindana na Paul Kagame ambaye ametawala kwa mingi toka kutokea kwa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 baada ya mauaji ya  alieykuwa rais wa nchi hiyo Juvenal Habyarimana kilichosababisha maujai ya kikabila kati ya wahutu na watusi.

Uchaguzi awamu hii umekuwa na shamsham nyingi hasa kutoka kwa wapinzani kutokana na vyama upinzani kujitokeza kwa wingi na kuweka wagombea wao,Wapinzani wamekuwa wakimlaumu kujilimbikizia kwa madaraka kwa Paul kagame ikiwemo na kubadili katiba ya nchi kwa kuongeza kipindi cha kukaa madarakani ili kuweza kumpa muda zaidi wa kuitawala nchi hiyo.

Leo ijumaa agosti 04 2017 wanyarwanda wameamkia kwa ajili ya kupiga kura kulikoanza saa moja asubuhi mapema ili kufanya maamuzi juu ya kiongozi wa kumuweka madarakani,kumekuwa na tetesi toka kwa wapinzani kuwa Kagame amekuwa rais dikteta na serikali yake inendeshwa kwa mabavu kwa kuukandamiza upinzani kwa kutumia vyombo vya dola.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanaona uchaguzi wa rwanda ni sawa na kiini macho tu kwani paul kagame ameweka mizizi mikubwa sana ktk dola hivyo hawezi achia madaraka kwa sasa.

Rwanda ni miongoni mwa nchi ya mashariki inayokuwa uchumi wake kwa kasi sana na kuboresha maisha ya wananchi wake.





Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KINDUMBWENDUMBWE CHA UCHAGUZI RWANDA CHAFIKA UKINGONI LEO"

Back To Top