
Rais Magufuli ameagiza kamati hiyo kuendelea kuhoji na kutafutawatu wote na viongozi waliohusika kwa njia moja au nyingine waliingiza taifa ktk aina hii mbaya ya mikataba ya madini iliyopelekea taifa kupata hasara kubwa ya kukosa mapato makubwa ya matrilioni ya shilingi kwa kushindwa kukusanya kodi kikamilifu .

Taasisi na vitengo mbalimbali vinavyohusika ktk uchimbaji na machakato mazima wa madini pia vimehusishwa na kuingizwa ndani ya sakata hili baada ya kushutumiwa kuwa kwa makusudi baadhi ya maofisa na wagfanyakazi wa serikali walihujumu jitihada za serikali kwa kundekeza maslahi yao buinafsi na kuiweka nchi mahali pabaya.

Rais ameapa kulisimamia jambo hili na mengine yote yanayohusisha ubadhilifu wa mali za ummana kamwe hatishi na wanasiasa wala makampuni yanayotaka kumshitaki kwa kisingizio kuwa anavunja mkataba,yeye hatishi na ameagiza makontena yote aliyoyazuia kamwe yasitoke mpaka pale Acacia watakapokaa na kukubaliana kulipa pesa zote wanazodaiwa na serikali,kujisajili brella na kuanza mchakato upya.

Serikali inaidai zaidi ya Trilioni 108 kamapuni ya Acacia kama kodi walizokimbia kwa miaka kadhaa ktk madini ya dhahabu pekee ambayo ni zaidi ya tani 1240.
Rais amesema mikataba hiyo yote itarudishwa bungeni kwa ajili ya kuijadili upya na kumuagiza spia wa Bunge Job Ndugai kusimamia kwa uimara na kuwaondoa wale wote watakaokuwa wanaropoka hovyo bungeni na yeye atawashughulikia kikamilifu endapo wataropoka wakiwa nje.
0 Comments "RIPOTI YA PILI YA MAKINIKIA:WALIO HUDUMU WIZARA YA NISHATI NA MADINI KUANZIA 1998 KUKIONA"