KAMATI YA PILI YA UCHUNGUZI WA MADINI (MAKIMIKIA) KUWAVUA MATAULO VIGOGO LUKUKI WA SERIKALI

Leo juni 12 2017 Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dk.John Joseph Magufuli anapokea taarifa ya kamati ya pili ya uchunguzi wa sakata la madini hasa kwa kampuni ya ACACIA inayofanya kazi zake ktk migodi mbalimbali duniani ktk uchimbaji wa madini.

Taarifa za awali za hivi punde zinazoendelea mda huu ikulu zinazowasilishwa na mkuu wa kamati hii ya pili ya uchunguzi wa madini ktk uchumi zimesema kuwa kampuni hii ya ACACIA inayohusika na uchimbaji na usafirishaji wa madini nje ya nchi kuwa haina leseni ya ya usajili ya kuchimba madini kutoka serikalini toka ilipoanzishwa mwaka 1998.

Kwa mujibu huu ACACIA haina uhalali wa kuwepo na kuchimba madini nchini,pia mkuu huyo wa kamati huii aliongeza kuwa viongozi na wafanyakazi wengi wa serikali wanaohusika na mambo haya ya madini wamekuwa wakitoa na kuandaa taarifa za uongo zinazohusiana na kuampuni hii ACACIA kwa kipindi chote cha utendaji kazi zake hapa nchini.

Pia imethibitika kuwa kampuni hii hailipi kodi halali kulingana na aina au kiwango cha madini wanachosafirisha kwenda nje,pia kamati imegundua kuwa kampuni hii haina idara ya fedha hapa ndani ya nchi ila Afrika kusini tu.


 Toka kuanza kwa shughuli za uchimbaji wa madini kampuni ya ACACIA mwaka 1998 wamesafirisha Tani nyingi za madini za aina mbalimbali yakiwemo dhahabu,shaba,lithiamu na hivyo kufanya serikali kupoteza trilioni za shilingi.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KAMATI YA PILI YA UCHUNGUZI WA MADINI (MAKIMIKIA) KUWAVUA MATAULO VIGOGO LUKUKI WA SERIKALI"

Back To Top