
Wandamu ni lazima ujifunze sana saikolojia ya kuishi na watu wa aina na tabia mbalimbali ili kuepusha migogoro ambayo endapo itaachiwa kukua bila kutafutiwa ufumbuzi haraka inaweza kuja kuzaa madhara makubwa kama vita,mauaji,chuki hata mifarakano ktk jamii.

''Kuficha taarifa zako zote za msingi kwa adui yako''
''Kujua taarifa zote za adui yako kwa kina na uhakika''
''Kufanya majadiliano na uchunguzi wa kina kabla ya kwenda kumkabilia adui yako''
''Si vyema kwenda kumkabili adui usiyemjua au kuwa na taarifa zake kwa kina''
''Ni vyema kuijua nguvu ya adui yako kabla ya kuanzisha mapambano''
''Pambana na adui huku ukiwa na hakika ya kushinda vita hiyo ili kuepuka kuwa mateka au mtumwa kwa adui yako pindi akishinda yeye''
''Ambush au njia ya kupiga kwa kushtukiza ni miongoni mwa njia nzuri za kushinda vita''
''Ni vigumu kushinda vita kwa kupambana na adui anayekujua wewe zaidi kwa mda mrefu kuliko wewe umjuavyo yeye''
''Ni vyema kuwa mpolea au subira zaidi inapobidi ili kusubiri upate nguvu za kupambana naye kuliko ukabahatisha kipindi ambacho wewe bado dhaifu''
''ikiwa wewe ni kiongozi wa kundi la watu basi ni vyema kutaka ushauri kwa watu wa karibu wenye busara kuliko kuchukua maamuzi ya peke yako''
Kumbuka:
Mataifa yote makubwa na yaliyoendelea ktk njanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi,kijamii,kijeshi,sayansi na kiteknolojia,wao walitumia njia za majadiliano na kutakana ushauri ktk kila hatua ya mandeleo ya mataifa yao.

wao wamekubali kuuacha mifumo na vitengo vifanye kazi zake na sio kubaki kama mapambo tu.
Wao utafuta taarifa za kina juu ya jambo lolote lile kabla ya kusema au kuamua kuchukua hatua na sio kukurupuka.
Wao upanga,kuratibu,kusimamia na kumua kufanya yale wanayokubaliana ktk mijadala.

''Nje ya hapo tutafeli kila siku''
0 Comments "MAJADILIANO NA KUTAKANA USHAURI NDIO NJIA PEKEE YA KUMSHIDA ADUI YEYOTE!"