TETEMEKO KUBWA LA ARDHI LATIKISA MEXICO

Zaidi ya watu 248 wameripotiwa kufariki dunia leo ktk jiji la Mexico city makao makuu ya Mexico baada ya tetemeko kubwa la ardhi kulitikisa jiji hilo kwa sekunde kadhaa.

Tetemeko hilo lenye nguvu za  kipimo cha Ritcher scale 7.1 ni miongoni mwa matetemeko makubwa kuwahi kutokea ktk mji huo,Majengo ya makazi,viwanda,maduka,ofisi na miundombinu mbalimbali imeharibiwa vibaya ktk jiji hilo,hali ya taharuki imewashika wakazi wengi wa jiji hilo kwa kuhofia kupoteza maisha yao na ndugu hasa baada ya watu wengi kuhisiwa kuwa bado wamefukiwa na vifusi vya majengo yalibomoka.

Tetemeko la ardhi ni miongoni mwa majanga ya kiasili yasiyowezekana kuzuilika kawa njia yeyote ila na njia za kibinadamu na mbaya zaidi uja kwa ghafla kabisa,tetemeko hili ni kubwa kabisa kuwahi kutokea ktk nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 32 ilyopita.




Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "TETEMEKO KUBWA LA ARDHI LATIKISA MEXICO"

Back To Top