KOREA KASKAZINI,IRAN ZAONYWA NA KUBEZWA NA MAREKANI

Rais wa marekani Donald Trump amembeza na kumuonya Kiongozi wa taifa korofi la korea kaskazin Kim Jong Un kwa kumwita (Rocket Man) au Mzee wa Makombola kuwa kama ataendelea na tabia yake ya kuogopesha na kuhatarisha amani ya marafiki zake Japan na Korea kusini kwa kuendelea kuvurumisha makombola kila kukicha ataivamia na kuharibu korea kaskazini na kuundoa uongozi wake  moja kwa moja.

Maneno haya makali yamesemwa na Rais Donald Trum akiwa ktk mkutano wa Umoja wa mataifa uliofanyika ktk jiji kubwa la New York lililopo nchini mwaka Marekani,pia ameionya Iran kwa tabia yake ya kuharibu usalama wa mashariki ya kati kwa kusaidia vikundi vya kigaidi vinavyovamia maeneo mengi na kutesa watu.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Guterres ameiomba dunia kuacha tabia ya dunia kugawanyika ktk swala la amani kwani kwa sasa hali ya usalama wa dunia umeshagawanyika ktk makundi mengi hivyo aliwaomba wanachama kuwa kitu kimoja kuwa mshikamano ktk swala la kuleta amani duniani.




Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KOREA KASKAZINI,IRAN ZAONYWA NA KUBEZWA NA MAREKANI "

Back To Top