Kimbunga kilichopewa jina la (Maria) kimepamba moto baada ya kuanza kupiga visiwa kadhaa vikiwemo vya Dominican Repulic,Haiti,Porto Rico na S.t Martin,Guadeloupe kwa mara ya pili baada ya siku chache tu kupitiwa na kimbunga Harvey na kufanya uharibifu mkubwa wa miundombinu na makazi ya watu karibu eneo zima la visiwa vya Carribean.
Nyumba na majengo mbalimbali yanaendelea kuharibiwa vibaya sana kutokana na mvua kubwa zilizosababisha kujaa kwa maji mengi mtaani,upepo mkali unaosafiri kilomita 260 kwa saa,Vimbunga hivi vya kitropiki vimekuwa vikitokea mara kwa mara ktk visiwa hivi ikiwemo na kile kilichotokea mwaka 1998 kilichoitwa kwa (George) na kuwaacha maelfu ya watu wakihangaika kutafuta vyakula na maji salama kwa ajili ya kuokoa maisha yao.
0 Comments "KIMBUNGA MARIA KUCHAKAZA TENA VISIWA KADHAA"