KIMBUNGA (IRMA) KUSAFISHA VISIWA ATLANTIKI

Kimbunga kikubwa ktk bahari ya atlantiki kilicopewa jina la IRMA AU (Hurricane IRMA) kimeitikisa marekani ya kusini na visiwa vyake baada ya kuharibu makazi,miundombinu kama barabara na kuwaacha watu zaidi ya miloni 9 wakiwa wako kizani,hawana maji safi na salama.

Kimbunga hiko kinachosafiri kwa kasi ya kilomita 300 kwa saa kimeharibu vibaya visiwa vya St. Martin,Barts,Barbuda,Haiti,Dominican,Bahamas,Jamaica,Cuba na maeneo mengine ya jirani,mvua kubwa zilizoambatana na pepo kali na radi zimekuwa zikivyesha usiku na mchana na kusababisha nyumba,barabara nyingi kufunikwa na maji hivyo kufanya mambo kuwa magumu zaidi kwa watu,huduma za maji,umeme,vyakula na makazi zimekuwa ngumu kupatikana.

Kimbunga hiki kinakisiwa kuelekea pande za peninsula ya California ktk siku zijazo,siku chache zilizopita jiji la Huston ktk jimbo la Texas limekubwa na balaa la mafuriko makubwa yaliyosababishwa na kimbunga Harvey nan kuleta uharibifu wa mabilioni ya dola.














Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KIMBUNGA (IRMA) KUSAFISHA VISIWA ATLANTIKI"

Back To Top