Kamati ambayo imeundwa na spika wabunge Joseph Ndugai na baadhi ya wabunge kutoka vyama mbalimbali ili kuchunguza mikataba na shughuli zote za uchimbaji na utoaji wa madini ya Tanzanite mkoani manyara na yale madini ya almasi ktk mkoa wa Shinyanga imekuja na ripoti iliyoibua makubwa zaidi ya zile ripoti za awali za Dk.Mruma wa makinikia ya dhahabu ya mgodi wa Acacia na ile ya Dk Osolo.
Ripoti hii iliyowasilishwa jana Dodoma kwa waziri mkuu na leo ikulu kwa rais Magufuli imetoa mambo mengi ya ubadhilifu wa mali za umma hasa ktk rasilimali madini.
Rais Magufuli leo ikulu ameipokea ripoti hiyo iliyowasilishwa na Mbunge wa Ilala Mussa Hassan Zungu,spika wa bunge Joseph Ndugai na baadhi ya wanakamati wengine waliopata nafasi ya kuzungumza mbele ya hadhara hiyo.
Baadhi ya mambo
yaliyozungumzwa ktk ripotui hiyo ni juu ya kusainiwakwa mikataba mingi ya madini ambayo imeiingiza nchi ktk unyonywaji wa hali ya juu na kupoteza mapato kwa kipindi kirefu,utoroshwaji wa madini madini kwa kiasi kikubwa bila wataalam wanauhusika kupima au bila kutopata taarifa,ulaji wa rushwa kwa kiasi kikubwa kwa watu waliowekwa ktk maeneo ya migodi na wanaoshughulikia maswala ya madini ili kuwafanya wasifuatilie taarifa za msingi kwa makusudi.
Ripoti imewataja viongozi na vigogo kadhaa walikuwepo na waliostaafu ambao walishiriki ktk jia moja au nyingine kwa kujua au kwa makusudi kabisa kuingia mikataba hiyo mibovu kabisa iliyoingiiza nchi ktk unyonywaji.
Waziri Simbachawene,Edwin Ngonyani ambao pia wameonekana kuwepo ktk sakata hilo wamejiuzulu leo hii ili kupisha uchunguzi zaidi juu yao kwakuwa wako ktk kashfa hiyo kubwa.
Ripoti imepokelewa kwa masikitiko makubwa na Rais Magufuli na kusema kuwa mambo anayoyafanya hafanyi kwa kubahatisha yeye ana taarifa kamili kabla ya kufanya haya yote tunayoyaona na kusikia hivyo anafanya akiwa na uhakika ili watanzania watambue taifa lao linavyoingizwa ktk lindi la umasikini kwa kusalitiwa na watanzania wenzao wasio wazalendo na wanaojali maslahi yao binafsi.
Aliongeza pia kuwa baadhi ya watu waliatajwa humo walikuwa na kazi maalum ya kuchunguza taarifa za msingi na kuzileta kwake rais hivyo lazima watatajwa na ripoti hiyo,Dk.Mruma ni miongoni mwa viongozi waliopewa kazi hiyo maalum,Rais alishapeleka watu wake ktk kila kona na idara mbalimbali kwa nia ya kumletea taarifa za msingi juu ya ubadhilifu huo wa mali za watanzania na tayari wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuleta taarifa nyingi za misingi.
0 Comments "JOPO LA NDUGAI LANG'OA VIGOGO SERIKALINI"