
Maji yana kazi nyingi na muhimu zaidi ktk dunia yetu kwani asilimia 71% ya uso wa dunia umezingukwa na maji yanaweza kuwa ya bahari,maziwa,mito,mabwawa,chemichemi yakiwa ktk hali ya chumvi au baridi,kuganda au kimiminika,isipokuwa asilimia 29% tu ya uso wa dunia ndio kuna nchi kavu yakiwemo mabara na visiwa.

Maji baridi kwa kiasi kikbwa ndio utumika ktk shughuli za kilimo,kunywa,kupikia,kufulia,kunyweshea wanyama na kazi mbali mbali ndiyo yanayo onekana adimu zaidi baada ya mabadiliko ya hali ya hewa kuendelea kujitokeza kwa kass kubwa kutokana na uharibifu wa mazingira,ukataji wa misitu,moshi wa sumu kutoka viwandani ambavyo vyote kwa pamoja vimekuwa ni sababu kuu za hali hii ya upotevu wa maji safi na salama kwa matumizi ya kibinadamu.

Nyanzo vingi vya maji safi ambavyo vilitegemewa sana na jamii vimepotea kwa kukauka ua kupungua kwa kasi kubwa,hali hii imepelekea migogoro ya kijamii na hata nchi kwa nchi kwa watu kushindwa kulima,kufuga na kufanya shughuli zinazotegemea maji kwa kiasi kikubwa.

Mimea,wanyama vyote kwa jumla vikionekana kufa na vyanzo vya maji kukauka baada ya mvua kutokunyesha kwa mda mrefu na kuwa na vipindi virefuzaidi vya jua kali.
0 Comments "UPUNGUFU WA RASILIMALI MAJI KULETA VITA AFRIKA,ASIA"