KOREA KASKAZINI WAUWASHA MOTO UPYA!

Korea kaskazini wamefytua upya bomu lililovuka nchi ya japan na kuanguka ktk  pembe ya mji wa Erimo Hakkaido na kuwastua raia wa japan kwa kuhisi sasa mashambulizi rasmi yameanza kama alivyoahidi kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un kuwa yuko tayari kupambana na yeyote yule atakayeonekana kutishia usalama wa taifa lake la korea kaskazini.

Bomu la safari hii limesafiri umbali wa kilomita zipatazo 2,700 km,hali hii imemfanya waziri mkuu wa japan Shinzo abe kuitisha kikao cha dharura ktk baraza la usalama la umoja wa mataifa (UN) ili kujadili hali ya hatari inayosababishwa na korea kaskazini mara kwa mara.

Jaribio hilo la bomu la masafa marefu lilifanyika majira ya saa 11:58 Mapema asubuhi ya leo jumanne,Marekani ikiwa kama mshirika mkubwa wa Japan Imeithibitishia kuwa kamwe iko karibu zaidim ktk usalama wa marafiki zake ikiwemo japan na korea kaskazini juu ya vitisho vyote wanavyofanyiwa na korea kaskazini.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KOREA KASKAZINI WAUWASHA MOTO UPYA!"

Back To Top