KIMBUNGA HARVEY KUHAMISHA WATU 30,000 TEXAS

Kimbunga kikali cha harvey hurricane kimeendelea kuvuma  na kufanya uharibifu mkubwa pwani ya kusini mashiriki mwa marekani kwa siku kadhaa na kusababisha watu zaidi ya 30,000 kuhama ktk makazi yao na kuelekea ktk majimbo mengine kuokoa maisha yao.

Jiji kubwa la nne kwa ukubwa nchni humo la Huston limeathirika kwa kiasi kikubwa na kimbunga hiko kilichoambatana na pepo kali pamoja na mvua kubwa zinazonyesha usiku na mchana.

Miundombinu ya umeme,barabara pamoja na makazi yameonekana kuharibiwa vibaya na kusababisha watu kukimbia makazi yao kwa kukosa huduma za msingi.

Dallas umeteuliwa kuwa mji maalum kwa kuwapokea na kuweka makazi kwa watu wote walioathirika na kimbunga hiko.


 Miundo mbinu ya umeme ikiwa imeharibiwa vibaya kwa upepo makali huku gari nayo ikiwa imetumbukia mtaroni baada ya dereva kukosea njia.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KIMBUNGA HARVEY KUHAMISHA WATU 30,000 TEXAS"

Back To Top