
Kagame anayeiongoza nch ya rwanda toka mwaka 1994 amekuwa akionekana kuwa ni kiongozi shupavu na mpenda maendeleo na wananchi walio wengi wa rwanda hasa kwa kuzuia machafuko ya kisiasa,kikabila na kuleta maendeleo ya haraka kwa kuweka nidhamu kubwa kwa serikali.
Zaidi ya wananchi milioni 5.4 ambao walikuwa ndio wapiga kura halali kwa uchaguzi huu,asilimia 98% ya wapiga kura hao wamepigia Paul Kagame.
Rwanda ni miongoni mwa nchi za afrika mashariki ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi zaidi licha ya nchi hiyo kuwa na ufinyu wa rasilimali kama ardhi,watu wamekuwa wakijitahidi sana kupiga hatua kwenye swala zima la kupeleka nchi yao mbele kimaendeleo.

0 Comments "PAUL KAGAME AIKAMATA RWANDA KWA MARA YA TATU BAADA YA KUSHINDA UCAHAGUZI KWA KISHINDO"