Jana ijumaa majira ya saa 12:00 jioni ndege ya Tanzania iliyokuwa ikitokea nchini uganda ikiwa imembeba rais wa nchi hiyo Mh.Yoweri Kaguta Museven ilitua ktk uwanja wa ndege wa majani mapana uliopo jijini Tanga ikiwa ni mataarisho ya siku ya leo jumamosi agosti 05 2017 ktk tukiola uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi unatarajiwa wa bomba la kusafirishia mafuta ghafi (Crude oil) kutoka ziwa albert lilopo nchini uganda kuja hadi ktk mkoa wa Tanga ktk kijiji cha Chongeliane.
Rais museven aliyepokelewa na waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na makamu wa rais Mama Samia Suluhu Hassan alikagua gwaride maalumu licha hali ya hewa ya jana kuwa na ya mvua kwa siku nzima yote.
Bomba hili la mafuta ghafi litakalokuwa na urefu wa zaidi ya kilomita 1,444 kutoka Uganda hadi Tanzania litagharimu zaidi ya dola bilioni nne ($4 )litachukua mda wa miaka mitatu hadi kukamilika huku kampuni kubwa ya mafuta ya TOTAL ya nchini ufaransa ikiwa ndio wajenzi wa bomba hilo,zaidi ya ajira 15,000 zitapatikana na zaidi ya ajira 2,000 za kudumu kati ya hizo zitaendelea kuwepo hata baada ya kumaliza ujenzi wake.
Rais magufuli alizungumzia mengi ikiwa ni kama faida ya ujio wa bomba hio ikiwemo kukuwa kibiashara kwa vijiji zaidi ya 114 vitakavyopiyiwa ni mradi huo,kupata ajira za mda,malipo kwa wale watakochukuliwa ardhi kwa ajili ya kupisha mradi huo,ikiwemo na kodi nyingi itakayokusanywa na serikali ikiwa kama malipo kwa nchi yetu.
Akiwa katikati ya mazungumzo rais Magufuli aliwasifia wanakikundi cha mziki cha Tanzania all stars kwa kuimba wimbo mzuri wa amani na uzalendo kwa nchi yao hii,akasisitiza kuwa uganda ni zaidi ya marafiki wao bali ni ndugu wa karibu sana kwani wamekuwa wakisaidiana kwa mengi toka wakatui wa vita ya kumuondoa Idd Amin 1978/79.
Ghafla alijikuta akimuita Mkurugenzi wa Clouds media Bwana Ruge Mutahaba kuja mbele kisha na kumuita tena Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na kusema "vijana hawa nawapenda sana wote hivyo nataka myamalize mambo yenu kuanzia leo" Rais Magufuli alisistiza kuwa wakumbatiane na kushikana mikonon wakati wakiwa wanaondoka ktk jukwaa hilo.
Hali hii imekuja ikiwa ni miezi kadhaa sasa baada ya shutuma za uvamizi wa clouds tv mikocheni kulikolalamikiwa na Clouds kuwa kulifanywa na mkuu wa Mkoa huyo,na kuleta mtafaruku mkubwa baina ya wanahabari wote kwa kusumsia mkuu wa mkoa huyo kwa kutokutoa habari zake za aina yeyote ile inayomuhusu yeye.
Home
» kitaifa
» JPM ANG'OA MZIZI WA FITINA KATI YA MAKONDA NA RUGE AKIWA KTK UZINDUZI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA TANGA
0 Comments "JPM ANG'OA MZIZI WA FITINA KATI YA MAKONDA NA RUGE AKIWA KTK UZINDUZI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA TANGA"