MUGABE AIONGOZA ZIMBABWE AKIWA NUSU MZIMU

Kwa miaka zaidi ya 37 sasa kutokea mwaka 1980 ambapo zimbabwe ilipata uhuru wake toka kwa wakoloni wa kingereza na kukabidhiwa kwa Robert Mugabe amekuwa akiingoza nchi hiyo kwa mda wote licha ya kufanya uchaguzi wa kidemokrasia mugabe amekuwa akishinda chaguzi zote.

Mugabe ambaye kwa mda mrefu sasa amekuwa akionekana kama dikteta wa afrika kwa kutawala mda mrefu zaidi nchi hiyo,Mugambe alifanya mabadiliko ya sheria za ardhi kwenye mwishoni mwa miaka ya 1990s. na kusababisha mgogoro mkubwa kati yake na wazungu wengi waliokuwa wakimiliki sehemu kubwa za ardhi na mashamba ktk nchi hiyo ndogo iliyobalikiwa ardhi yenye rutuba.

Kwa sasa Mugabe yuko mbioni ktk kampeni za uchaguzi kwa ajili ya kujiweka tena madarakani licha ya hali yake ya kiafya kuwa mbaya kutokana na umri mkubwa alionao wa miaka 93 toka kuzaliwa kwakwe februari 21-1924.

Mugabe mara kadhaa amekuwa akianguka ktk mihadhara,akisinzia mara kwa mara na kutoonekana ktk mikutano mikubwa badala yake kuhudhuria mkewe Bi.Grace Mugabe ambaye ndio anayempigia kampeni.

Robert Mugabe ameapa kuingoza Zimbambwe hadi pale kifo kitakapomkuta.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MUGABE AIONGOZA ZIMBABWE AKIWA NUSU MZIMU"

Back To Top