MUGABE KUFA KISHUJAA KWA KUJENGA CHUO KIKUU KWA DOLA BILIONI MOJA

Ktk hali ya kuonyesha kuwa nchi ya zimbabwe kamwe haitopiga magoti kwa wazungu ili kuomba na kupata misaada ya kimaendeleo ya nchi hiyo,Rais Robert Mugabe ameuthibitishia umma kuwa nchi yake iko imara baada ya kutangaza kuwa wanatarajia kuanza ujenzi wa chuo kikuu kikubwa kabisa ndani ya nchi hiyo kitakachotumia gharama za Dola bilioni moja  za kimarekani ($1 bilion) ktk ujenzi wake.

Chuo hicho kitakachopewa jina la kiongozi huyo mkongwe kabisa barani afrika mwenye umri wa miaka 93 sasa kitakuwa na jina la ROBERT MUGABE UNIVERSITY,kitakachojengwa ktk mji wa Mazowe nje kidogo mwa jiji la Harare .

Wataalam wa mambo ya uchumi wanahoji na kushangazwa kuwa uchumi wa nchi hiyo kwasasa umetetereka sana toka mwaka 2000,sasa ni wapi au vyanzo gani vitakavyowezesha kupata pesa yote nyingi kiasi hiko kwa mapato ya ndani pekee.




Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MUGABE KUFA KISHUJAA KWA KUJENGA CHUO KIKUU KWA DOLA BILIONI MOJA "

Back To Top