KOREA KASKAZINI KUSHAMBULIA KISIWA CHA GUAM ILIPO KAMBI YA KIJESHI YA MAREKANI

Jana  jumatano kituo cha runinga cha taifa cha korea kaskazini KCNA ilitangaza juu ya azma yake ya kuanza mataarisho ya kuishambulia kambi ya kijeshi ya marekani iliyokuwepo ktk kisiwa cha Guam ktk Bahari ya pasifiki kutokan na ishio la uwepo wake karibu na nchi yake.

Rais wa marekani Donald Trump ameionya korea kaskazini juu ya kauli hiyo kuwa endapo watajaribu kufanya hivyo basi watakuwa wamechokoza moto ambao hawatoweza kuuzima kamwe na watajutia kwa maamuzi hayo ya kigaidi watakayodiliki kuyafanya.

Korea kaskazini imeapa kuwa ina mpango wa kutumia makombola yake ya masafa ya kati ktk kuishambulia kambi hiyo ya wana maji iliyopo ktk kisiwa hicho cha Guam iliyopo umbali wa kilomita 3,402 kutoka mji mkuu wa pyongyang.

Kiongozi wa taifa hilo la kijamaa Kim Jong Un amekua akiarimsha kufanyika kwa majribio mengi ndani ya mwaka huu pekee ambayo yote amekuwa akiyaelekeza nchi za Japan na Korea kusini na mengine kusafiri umbali wa kilomita 4,100.




Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KOREA KASKAZINI KUSHAMBULIA KISIWA CHA GUAM ILIPO KAMBI YA KIJESHI YA MAREKANI"

Back To Top