Baadhi ya nchi kama Uingereza,ubelgiji,uswizi wamepiga marufuku uingizaji wa mayai kutoka uholanzi na kufanya juhudi za makusudi kuyaondoa mayai yote ambayo yameshaingizwa na kusambazwa ktk masoko mbalimbali ktk nchi hizo ili kuepusha watu kununua n kuyatumia mayai hayo yenye sumu.
Kashfa hii ya kuingiza mayai yenye sumu ktk masoko ya dunia si ya mara kwanza kwani ndani ya kipindi hiki cha miaka miwili Ujerumani iliwahi kupata shutma hizi za kuingiza mayai yenye sumu aina ya Fripnol ambayo hutumika kupuruzia ktk nyumba za ufugaji ili kuepusha kuku hao kupata viroboto ambao huwaletea magonjwa au kuwaandama kuku hao hadi kupoteza uhai.
Uholanzi ikiwa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa ufugaji wa wanyama na ndege wa aina nyingi,inazalisha zaidi ya mayai bilioni 11 kwa mwaka ambayo soko kubwa la mayai hayo ni barani ulaya,uingereza pekee wameingiza mayai hayo yenye sumu yapatayo laki saba (700,000).
0 Comments "MAMILIONI YA MAYAI YENYE SUMU TOKA UHOLANZI YAPIGWA MARUFUKU BARANI ULAYA"