MLIMA WAPOROMOKA NA KUFUKIA WATU 1000 SIERRA LEONE

Baada ya mvua kubwa kunyesha usiku na mchana ktk nchi ya Sierra leone iliyopo pwani bahari ya atlantiki magharibi mwa bara afrika,watu wapatoa 400 wamefariki dunia baada ya makazi ya watu yaliopo jirani na mlima kufukiwa na tope zito liliporomoka ghafla kutoka ktk mlima huo baada ya mvua kubwa kunyesha na kulegeza ardhi ya mlima huo.

Watu zaidi ya 600 wanahofiwa kufukiwa ktk vifusi vikubwa vya tope,mchanga na mawe,myuma na majengo mengi yalipo jirani na mlima huo yamefukiwa na kuharibiwa vibaya,idadi hiyo ya watu 1000 ambayo ni makisio tu inatisha na kufanya nchi hiyo kuomba msaada mataifa na mashiriki ya nje ya kuja kusaidia balaa hilo lililojitokeza ghafla ktk mji mkuu wa nchi hiyo wa Freetown.

Hii si mara ya kwanza kwa milima kukatika na kufunika miji na vijiji ktk maeneo mbalimbali ya miinuko kama ilivyojitokeza huko uganda,milima uweza kuporomoka kutokana na mvua kubwa za mda mrefu au baada ya matetemeko ya ardhi kutikisa milima hiyo na kujiachia sehemu yake.

Sierra leone ni miongoni mwa nchin masikini sana duniani baada ya kuathiriwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyopiganwa mdsa mrefu hadi kwisha,nchi hii ni tajiri kwa kuwa na rasilimali ya madni ya almasi kwa kiasi kikubwa.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MLIMA WAPOROMOKA NA KUFUKIA WATU 1000 SIERRA LEONE"

Back To Top