Tajiri namba moja duniani Bill gates mwenye umri wa miaka 61 kwasasa amekutana na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli siku ya tarehe 10/8/2017 na kutoa msaada wa fedha zaidi ya dola za kimarekani shilingi milioni 350 sawa na pesa za kitanzania shilingi bilioni 777.
Pesa hizo ambazo zimetolewa kupitia taasisi yake ilipo nchini humo ya Bill anda Melinda foundationi yenye makao makuu nchini marekani,pesa hizi zinzkusudia kuelekezwa ktk miradi ya afya,kilimo,kukabiliana na vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi,kuondoa ugonjwa wa malaria,kupunguza utapi mlo n.k.
Bepari huyu mwenye kumiliki kampuni kubwa ya kutengeneza na kuuza Talakilishi na viwezeshi vyake maarufu kama Microsoft amesema ameridhishwa na utendaji kazi wa rais Magufuli hasa kwa kuzibiti mapato,kupunguza ubadhilifu,kusimamia mapato ya ndani,kupunguza rushwa,hasa ktk dhana yake ya utumbuaji majipu.
Bill gates ndio tajiri namba moja akifuatiwa na Warren Buffet kama tajiri nambari mbili kwa kumiliki kiasi kikubwa cha fedha n mali duniani.
0 Comments "BEPARI NAMBA MOJA DUNIANI BILL GATES ATOA MSAADA WA BILIONI 777 KUSAIDIA TANZANIA"