Je wajua! kuwa mamilioni ya watu duniani wanazaliwa na kufa kila sekunde ipitayo ktk saa yako! ukweli ndio huu kuwa watu wengi upoteza uhai na kuzaliwa kwa kila saa na siku ipitayo ktk maisha yetu.
Wataalam wanatueleza kuwa asilimia kubwa ya vifo duniani inatokana na magonjwa ya aina mbalimbali ambayo uwapata wanadamu na kuwasababisha uharibifu wa maumbile na kutokufanyika kwa uzuri kazi za mwili kunakosababisha utendaji dhaifu wa mifumo ya mwili wa mwandamu.
Magonjwa yamekuwa yakichukua nafasi ya kwanza ktk kuua watu wengi duniani,magonjwa haya baadhi ni yatokanayo na tabia na maisha halisi ya mtu husika na mengine yanatokana na na maambukizi kutoka ktk vimelea vya maradhi kama virusi na bakteria.
Baadhi ya magonjwa haya kama ukimwi,kifua kikuu,kansa,magonjwa ya mifumo ya upumuaji,njia za chakula,malaria,ila wataalam wanatuelez magonjwa yanayo ongoza kwa kuua zaidi duniani ni yale ya kansa ya mapafu,kansa ya koo,kisukari,na presha au shinikizo la damu.
Zipo sababu nyingi sana zinazoweza kusababisha kifo kwa mwandamu kama ajali za vyombo vya usafiri,viwandani au sehemu mbalimbali za kazi,sababu nyingine ni zile za kukusudia kama kuuwawa kwa sumu,kupigwa n.k lakini licha kuwepo sababu hizo bado magonjwa ndio yanashika nambari moja ktk kuuuwa watu.
Tafiti za wataalam wa mambo ya kibinadamu zinasema kuwa ktk kila watu 1000 uzaliwa watoto 19 na ktk kila watu 1000 ufariki watu 8.
Ktk mwaka mmoja uzaliwa watoto wapatao milioni kumi na tatu na laki nne 13.4 lakini pia ufariki watu milioni hamsini na tano na laki tatu 55.3.
Kwa kila siku moja duniani uzaliwa zaidi ya watoto laki tatu na sitini elfu 3,60000 na ufariki watu laki moja na hasini na moja elfu na mia sita 151600.
Kwa kila saa moja ipitayo watoto elfu kumi na tano 15,000 na ufariki zaidi ya watu elfu sita mia tatu na kumi na sita 6,316.
Kwa kila dakika moja watoto 250 na ufariki zaidi ya watu 105
Kasi hii ya tafiti baina ya kifo na uhai inaonyesha kuwa bado kasi uzalianaji kwa wandamu iko juu zaidi mara mbili zaidi ya ile ya watu wanaokufa kwa kila nyakati. na hii ndio maana unaweza kuona hakuna tofauti kubwa uionayo hata baada ya watu wengi kufa kila siku kutokana na hali hiyo ya idadi ya watu wanaozaliwa kuwa mara mbili ya ile ya wanaofariki.
Makadirio ya maisha au uhai wa kuishi kwa mtu duniani ni miaka 67 licha ya hali kutofautiana baina ya nchi moja nanyingine kutokana aina ya huduma za kijamii na hali ya kipato cha wananchi husika na sababu nyingine mbalimbali kama nilivowahi kuandika ktk makala yangu za huko nyuma za SABABU NA JINSI YA KUEPUKA KUZEEKA HARAKA.
0 Comments "TAMBUA HII:NANI ZAIDI BAINA YA UHAI NA KIFO (JE WAJUA KUWA MAGONJWA NDIO SABABU KUU YA VIFO VINGI DUNIANI !)"