UHURU KENYATTA AZINDUA TRENI YA MWENDOKASI (MADARAKA EXPRESS)I KUTOKA NAIROBI KWENDA MOMBASA

Raisi wa kenya Mh.Uhuru Kenyatta jana mei 31 2017 amezindua Treni ya kisasa (Standard Guage) itakayotoka mji wa pwani ya mombasa hadi mji mkuu wa nchi hiyo wa Nairobi.

Treni hii itakayotembea zaidi ya kilomita 441 sawa na maili 274 kwa kutumia saa 4 na dakika 19 kwa kutumia usafiri huu wa kisasa kutoka mombasa hadi Nairobi.

Treni hii ya abiria maarufu kwa jina la MADARAKA EXPRESS itakuwa na uwezo wa kubeba watu wapatao 1260 kwa pamoja kwa bei ya Ksh 700 kwa ngazi ya kawaida na kwa wale wa mabehewa ya ngazi za juu ni Ksh 3000 tu.pia itakuwa ikifanya safari mbili kwa siku.

Mradi huu wa wa ujenzi wa reli mapak kukamilika umetumia pesa za Ksh bilioni 327 ambazo sawa na Dola bilioni 3.8 za kimarekani.

Pia kutakuwepo na treni maalumu kwa ajili ya kubeba mizigo ya kiabishara





Kuzinduliwa kwa mradi huu muhimu zaidi kwa tiafa la kenya kuna matarajio makubwa ya kiuchuni hasa kwa wafanya biashara ktk kusafirisha mizigo kutoka bandari ya mombasa hadi mji wa kibiashara wa nairobi hivyo kuongeza kazi ya kukua kiuchumi kwa mtu mojamomoja hadi kitaifa.

.







Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "UHURU KENYATTA AZINDUA TRENI YA MWENDOKASI (MADARAKA EXPRESS)I KUTOKA NAIROBI KWENDA MOMBASA"

Back To Top