ALIYEKUWA MBUNGE WA ZAMANI WA MOSHI MJINI PHILEMON NDESAMBURO AFARIKI DUNIA GHAFLA

Mwanachama na kada wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ndugu Philemon Ndesamburo aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la moshi mjini mkoani Kilimanjaro amefariki dunia ghafla jana kwa Mstuko wa moyo.
Ndesamburo ambaye ni maarufu kwa mkoa wa kilimanjaro na Arusha kutokana na Kujishugulisha na Biashara nyingi ktk miji hii miwili.

Alianza harakati za ubunge toka mwaka 2000 kupitia chama cha chadema na kushikilia jimbo hilo kwa miaka yote mpaka pale alipoamua kustaafu kazi hiyo mwenyewe.

Philemon alizaliwa februari 19 1935 na kufariki akiwa na umri wa maika 82.

Kabla ya kufikwa na umauti Ndesamburo alikuwa ktk harakati za kusaini hundi ya fedha za mchango wake kwa ajili ya kutyoa rambirambi za ajali ya shule ya Lucky Vincent iliyopo mkoani arusha,lakini pia alihudhuria mkutano wa chama cha chadema ulifanyika hivi karibuni mkoani Dodoma.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "ALIYEKUWA MBUNGE WA ZAMANI WA MOSHI MJINI PHILEMON NDESAMBURO AFARIKI DUNIA GHAFLA"

Back To Top