TRUMP:MAREKANI YAJIBU MAPIGO YA KOREA KASKAZINI KWA KURUSHA KOMBOLA LA MASAFA MAREFU ZAIDI

Uongozi wa kijeshi wa marekani umeamua kujibu mapigo ya kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un ambaye mara kwa mara amekuwa akifanya majaribio ya makombola yake ya masfa marefu akiwa na kusudio la kupata kombola litakalofika  marekani ikiwa litapigwa kutoka nyumbani kwake.

Hata hivyo mbio hizo za taifa hili la kikomunisti bado hazijafanikiwa kwani ndio kwanza wana makombora yanayotembea umbali wa kilomita 1000 tu hivyo kufanya kuzidisha juhudi zaidi ktk kukamilisha mpango wao huo wa kupata kombola la kinyulia litakalo ifikia marekani hasa mji mkuuwa Washinnghton.

Jana jumatano Jeshi la majini la marekani Us Navy limefanya majaribio la kombola lao ambalo lilifanikiwa kusafiri umbali wa kilomita 6700 kuelekea mashariki mwa bahari ya Pasifiki kuelekea visiwa vya hawaii, hata hivyo jaribio la mwaka 1990 la kombola la Sineva lilifanikiwa kusafiri umbali wa kilomita 11,547.

Marekani imewekeza zaidi ya dola bilioni 40 toka mwaka 2002 ktk ugunduzi huo wa makombola ya masafa marefu intercontinental ballistic missile ( ICBM) na mtambo wa kuzuia makombola ya masafa marefu THAAD.

Jaribio hili la jana limeigharimu serikali ya marekani zaidi ya dola milioni 244 nakusema mwezi agosti au septemba wanatarajia kufanya majaribio mengine tena ktk bahari hiyo ya pasifiki.

Kombola likijaribiwa jana.

 Moja ya kituo cha rada ya kijeshi kinachoelea baharini kinachomilikiwa na jeshi la marekani kwa ajili ya wasiliano ya kijeshi

Mtambo THAAD ukiwa tayari kwa kuharibu na kusambaratisha bomu lolote litakoloelekezwa kwao.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "TRUMP:MAREKANI YAJIBU MAPIGO YA KOREA KASKAZINI KWA KURUSHA KOMBOLA LA MASAFA MAREFU ZAIDI"

Back To Top