MWANAFUNZI WA KIMAREKANI ALIEACHIWA SIKU CHACHE KUTOKA KOREA KASKAZINI AFARIKI

Siku chache tu baada ya kuachiwa kwa kijana mwanafunzi Otto Frederick Warmbier aliachiwa hivi karibuni  kutoka ktk mikono ya utawala wa kikomunisti wa korea kaskazini chini ya Kim Jong Un baada ya kushikiliwa zaidi ya miezi mwaka mmoja na nusu kwa kile kinachosemwa kuwa kijana huyo alikuwa kaijaribu kufanya vitendo vya kauhatarisha usalama wa nchi yao hiyo ambayo inaendeshwa kwa sheria kali na ulinzi wa hali ya juu ktk mambo ya kiserikali.

Kijana huyo amefariki jana akiwa marekani ambapo ndio nyumbani kwao baada ya kuonana na wazazi wake ikiwa ni siku chache tu toka kuachiwa kutoka ktk utawala wa korea kaskazini.

Korea kaskazini ni nchi isiyewaamini watu wa marekani kabisa kuwepo ndani ya nchi hiyo kwa kuhisi au kudhania kuwa wanaweza kuwa ni majasusi au makachero wa serikali ya marekani ktk vitengo vya NSA,FBI,CIA ambao wako nchini kwa jaili yaudukuzi wa taarifa za muhimu kwa serikali ya korea kaskazii na kuzipeleka marekani.




Otto alirudishwa marekani toka korea kaskazini akiwa ktk ahali mbaya inayoonyesha alikuwa akipata mateso makubwa ya kupigwa na kuafanya kuwa na matatizo ya ubongo wake baada ya kuathirika kutokana na mateso hayo makali aliyokuwa akiyapata.


Rais Donald Trump amesema utawala wa korea kaskazini ni tishia kwa amani ya dunia na hata kwa vijana wasio na hatia kwa kuendeleza sera zake za kibabe na kidhalimu kwa watu wa marekani na duniani kwa ujumla,aliongeza kuwa yeye binafsi amesikitisha na taarifa hizo ila wataandaa jinsi ya kupambana na utawala huo wa kidhalimu (Brutal Regime).

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MWANAFUNZI WA KIMAREKANI ALIEACHIWA SIKU CHACHE KUTOKA KOREA KASKAZINI AFARIKI"

Back To Top