NINI UMUHIMU WA KUWA NA UTITIRI WA SIKU HIZI DUNIANI IKIWA MATATIZO NDIO KWANZA YANAONGEZEKA!

Sipingi wala sidharau juu ya uwepo utitiri wa masiku Maalum ya kuazimisha mambo mbalimbali duniani!
Ikiwemo magonjwa,haki za kibinadamu,misaada,elimu na kujitambua!
Nafahamu zimewekwa mahsusi kwa ajili ya kukumbusha watu juu ya mambo hayo!
Nachojiuliza ni kwa jinsi gani uwepo wa siku hizi lukuki ktk mwaka mmoja wenye Siku 365 1/4 zimeweza kusaidia makundi hayo husika yaliolengwa ikiwemo,wazee,akina mama,watu walibanwa ktk haki licha ya kuazimishwa kila mwaka!


Licha ya kuwepo kwa utitiri wa Siku hizi ambazo nyingi zake ziko chini ya Umoja wa mataifa UN hivyo kuzilazimu nchi zote wanachama wa umoja huo kufuta na kuzitambua siku hizo.
Kiukweli licha kuwepo kwa wingi wa siku hizo Maalum zilizotengwa bado dunia inahangaika na kuonhezeka,kusambaa kwa idadi ya magonjwa,Vifo kwa wakina mama wajawazito,ongezeko la idadi ya wakimbizi kunakotokana na vita ktk matifa mbalimbali.
Uvamizi na ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu kwa watoto,wakina mama,wazee ktk nchi zenye vita.


Kuendelea kwa mila potofu,ongezeko la mimba za utotoni,idadi kubwa ya wanoacha shule.
Kuongezeka kwa umasikini,ufukara,magonjwa ya akili yanayo sababishwa na maisha magumu,misongo wa mawazo,vipigo ktk ,mahusiano,ndoa,mauaji ya kiholela.
Nionacho Mimi si mbaya kuwa na Siku hizi Ila kikubwa kinacho hitajika ni juu ya kuichukua hata za kweli za kumaliza aua kupunguza matatizo hayo yanayowakuba watu,mazingira na sio kuweka masiku ya kumbukumbu kibao yasiyo na tija!


Tuache maisha ya kuogopana na kubaguana kisiasa,rangi,kikabila,dini,eneo na hata kiuchumi ili tuweze kufanya dunia yetu kuwa salama zaidi na sio kubagua mataifa yenye nguvu kupanga,kuamua na kufanya watakayo na kuwaacha wanyonge wakiteseka wasijue la kufanya!









"KUJUA KWAKO PEKEE KUWA JIRANI YAKO ANAUMWA SIO MSAADA UTAKAWEZA KUMUONDOLEA MAUMIVU AU UGONJWA BALI KWENDA NA KUTOA MSAADA WA MAWAZO,TIBA NA MALI NDIO UTATUZI WA YANAYOMSIBU"

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "NINI UMUHIMU WA KUWA NA UTITIRI WA SIKU HIZI DUNIANI IKIWA MATATIZO NDIO KWANZA YANAONGEZEKA!"

Back To Top