Bandari yetu ya Dar es salaam ambayo ndio iyotegewa na nchi hii kwa kuingiza mapato mengi zaidi ktkt serikali kutokana na kuingiza na kutoa kwa mizigo mingi kutoka nchi mbalimbali duniani na kusambaza ndani ya nchi na kupeleka nchi za jirani kama rwanda,burundi,uganda,kongo Drc,zambia na malawi kwakuwa nchi hizi hazina bahari hivyo kulazimika kuagiza kusafirisha na kuagiza mizigo yao kupitia bandari ya Dar es salaam tu kutokana na ukaribu wake.
Licha ya umuhimu wa bandari hii ya Dar es salaam kwasasa baada ya kupanuliwa na kuongezwa kina chake ndio ina uwezo wa kuingiza meli yenye uwezo wa kubeba kontena 4,000 za futi 20 tu na si zaidi ya hapo,ukubwa huu wa meli ya kontena 4,000 ni meli ndogo sana ukilinganisha na bandari nyinginezo duniani.
Kuna aina kuu mbili za bandari ambazo ni Za kiasili kama ya Mtwara ambayo iana kina kirefu zaidi kuliko bandari zote za nchini,aian ya pili ni Bandari za kuchimba kama ya Dar es salaam,Bandari za kiasili mara nyingi huwa na kina kirefu hivyo kuwa na uwezo wa kuingiza meli kubwa zaidi na zenye mizigo mizito kuliko bandari za kuchimba au kutengenezwa.
Zifuatazo ndizo bandari kubwa na zilizo bize zaidi kwa kuingiza meli kubwa na mizigo mingi zaidi duniani kote,Bandari hizi zenye uwezo wa kuingiza meli zenye uwezo wa kubeba hadi kontena elfu 19000 kazi zake uendesha kisasa zaidi na zina mitambo ya mawasiliano,ulinzi,upakuaji na upakizaji wa mizigo kwa haraka zaidi kuliko bandari yeyote duniani:-
1.SHANGHAI CHINA-ndio bandari ya kwanza kwa ukubwa na kuingiza mizigo iapatayo tani milioni 744 kwa mwaka,bandari hii ina ukubwa wa kilomita za mraba zipatazo 3,619.
2.NINBO-ZHOUSHGAN-CHINA
3.SINGAPORE
4.ROTTERDAM-NATHERLANDS
5.TIANJIN-CHINA
6.GUANGZHOU-CHINA
7.QINGDAO-CHINA
8.QUINHUANGDAO-CHINA
9.HONG KONG-CHINA
10.BUSAN-KOREA KUSINI
Unaweza kushangazwa kuwa bandari nyingi zaidi zilizo kubwa na zinazosafirisha mizigo mingi zaidi duniani zinapatikana china,ni ukweli kuwa kwasasa china ndio taifa pekee linasafirisha na kuingiza mizigo mingi zaidi duniani kuliko taifa lolote lile,kwa idadi hiyo ya mizigo ni wajibu kwa china kuwa na bandari kubwa,nyingi na za kisasa zaidi ili kurahisisha usafirishaji huo wa mali za watu,serikali na mashirika mbalimbali ktk nchi tofauti ulimwenguni kote.
Kwa bara la ulaya bandari zilizo kubwa zaidi na kuwa bize zaidi ni;-
Rotterdam ya uholanzi
Antwerp ya ubeligiji
Hamburg ya ujerumani
Amterdam ya uholanzi
Marssaille ya ufaransa
Le harve ya ufaransa
Prymorsk ya urusi
Bremen ya ujerumani
Bergen ya Norway
1 Comment "ZIJUE BANDARI KUBWA,ZINAZOFANYA KAZI KISASA NA KUINGIZA MELI KUBWA NA NYINGI ZAIDI DUNIANI"
If we constructing bagamoyo port will be the best