KIBURI CHA TRUMP CHADHIRIKA BAADA YA KUPANGA KUJIONDOA KWENYE MAKUBALIANO YA KUPUNGUZA UCHAFUZI WA HALI YA HEWA

Jeuri na kiburi cha raisi wa marekani Donald Trump kinazidi kuonekana baada ya kutaka kufanya mpango wa kuitoa marekani ktk mikataba ya kyoto na Paris iliyohusu kwa nchi zilizoendelea kiviwanda duniani kupunguza kiasi cha uchafuzi wa anga na mazingira kwa kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa (Carbondioxide) na hewa nyinginezo ambazo ni za sumu na ni hatari kwa mimea na viumbe vyenginevyo.

Mabadiliko haya ya hali ya hewa yameanza kuonekana kwa kasi zaidi kwa miaka hii ktk sehemu mbalimbali za dunia baada ya kujitokeza kwa athari zake kama kuwepo kwa ukosefu wa mvua kwa mda mrefu baadhi ya maeneo,kuwepo kwa mvua nyingi kiasi cha kuleta mafuriko,ukame na uaharibifu wa mazao kwa kunyesha kwa mvua za asidi au sumu,kufa na kupotea kwa baadhi ya viumbe,kupotea kwa visiwa kutokana na kujaa kwa maji baada ya barafu kuyeyuka huko aktiki,antaktika na maeneo ya milimani baada ya joto la dunia kuongezeka kwa kiwango kikubwa.

Nchi kama marekani,china,india,japan,ufaransa,uingereza,ujerumani,italia,urusi,korea kusini ndio mataifa yalikuwa na kiasi kikubwa kwa mchango mkubwa ktk kuchafua dunia kutokana na kuwepo kwa viwanda vingi vinavyotumia kiasi kikubwa cha makaa ya mawe,mafuta mazito ktk kuzalisha nishati za kuendesha viwanda hivyo ktk kuzalisha bidhaa mbalimbali,aina hii ya ambayo hutoa kiasi kikubwa cha hewa ukaa ambayo uenda na kukaa ktk anga na kuathiri.

Mataifa haya kwa kuona hali hiyo ya hatari zaidi inainyemelea dunia kwa kasi ziliamua kwa pamoja kukubaliana na kamua kuweka mikakati ya kuzuia hali hiyo isitokee au kuendelea tena.

Rais wa marekani Donald Trump ameishangaza dunia na wanachama wenziwe baada ya kutamka wazi kuwa yeye anafanya mpango wa kuiondoa marekani ktk makubaliano hayo ya Paris na kyoto hivyo hii imewastajabisha wengi kwani inakuwaje Taifa kubwa kama marekani lenye viwanda vingi na kuchangia kwa kiasi kikubwa cha uchangiaji ktk uchafuzi wa mazingra ya dunia kutaka kujiondoa ktk mikakati hiyo ya muhimu.

Viongozi wa mataifa mbalimbali wametoa yao wa mioyoni na kusema anachofanya mwenzao wamesikitishwa sana na wanashangazwa sana kwa taifa kubwa kama marekani kushindwa kufahamu umuhimu wa hali ya hewa ya dunia.






Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KIBURI CHA TRUMP CHADHIRIKA BAADA YA KUPANGA KUJIONDOA KWENYE MAKUBALIANO YA KUPUNGUZA UCHAFUZI WA HALI YA HEWA"

Back To Top