
Toka kutangazwa kwa kuondolewa kwa watumishi wa sekta za umma zaidi ya 9,932 kwa kuonekana wanatumia vyeti vya kughushi ktk taaluma zao hizo,Hali hii imeleta taharuki kubwa kwa sekta za elimu na afya kwa kuonekana upungufu wa watumishi ktk shule na hospitali mbalimbali nchini kwa watumishi hao kukimbia vituo vyao vya kazi ghafla bila kuaga na kuacha pengo kubwa ndani ya maeneo yao ya kazi.

Ndani la jiji la tanga mpaka sasa zaidi ya walimu 53 hasa shule za msingi wameripotiwa kukimbia kazi zao na kutokomea kusikojulikana,pia ktk manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wauguzi 31 kati ya 200 wa hospitali ya mkoa wameripotiwa kukimbia kituo hiko cha kazi kwa kuhofia kukamatwa na kupelekwa mahakamani.

Agizo la Rais Magufuli la kuwataka watu wote walioko ndani ya orodha ya watumishi wenye vyeti vya kughushi kuondoka haraka kabla ya mei 15 ili kuepuka kukamatwa na kfunguliwa kesi hatimaye wanaweza kufungwa miaka 7 kwa makosa hayo.

Hali hii imeleta sintofahamu kwa baadhi ya watumishi hao wa umma kwa kuona majina yao ndani ya orodha hiyo na kudai kuwa wao wanamiliki vyeti halisi vyote, wengi wao wamebaki wamechanganyikiwa wasijue la kufannya kwa kuogopa kukamatwa na kukosa mshahara wa mwezi mei.
0 Comments "WEMBE WA VYETI VYA KUGHUSHI (FEKI) WAZITESA SEKTA ZA ELIMU NA AFYA"