MVUA ZA MASIKA ZA MWISHO ZALETA MAAFA NCHINI

Mvua zinazoendelea kunyesha nchini kwa kipindi kirefu zimeleta maafa makubwa kwa makazi,mifugo na mashamba ktk maeneo mbalimbali nchini baada ya kuripotiwa kwa uharibifu wa zaidi ya hekari 1,500 za mashamba ya mpunga na mazao mengineyo mkoani Morogoro ktk wilaya ya Kilombero.







Kadhia hiyo iliyowaacha wakulima wa eneo hilo ktk wakati mgumu baada ya kuilamu mamlaka ya umiliki wa bwawa la kuzalisha nguvu za umeme la kihansi kuhisiwa kuwa wao ndio walioruhusu maji maengi kuingia ndani ya mashamba ya watu baada ya kuyafungulia pale wanapogundua yamekuwa mengi zaidi.






Hata hivyo uongozi wa bwawa hilo umepinbga malalamiko hayo na kusema kuwa kiasi cha mvua zinazonyesha ni kikubwa ktk maeneo mbalimbali kuzunguka eneo hilo lote ndio sababu kuu ya maji mengi kuingia mashambani na kufunika mashamba hayoKtk miji na majiji kama Dar es salaam  pia zimeleta balaa kubwa kwa wakaazi wa maeneo hayo baada ya kufunika baadhi ya barabara nyingi za miji,nyumba na ofisi mbalimbali kutokana na miundombinu duni inayoshindwa kuruhusu maji kupita na kuelekea sehemu husika.

Hali hii inaogopesha na kutishia uhai wa watu na hata kuleta uharibifu kwa mazao yaliyopo mashambani kufunikwa au kuzolewa kabisa na maji hayo yatembeyo kwa kasi,lakini pia kwa maeno mengi ya vijijini hasa ktk wilaya za pembeni barabara zake kuharibika kwa kiasi kikubwa kiasi cha gari kushindwa kupita na kuleta adha kwa wasafiri kulala njiani baada ya magari mengi kunasa.



















Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MVUA ZA MASIKA ZA MWISHO ZALETA MAAFA NCHINI"

Back To Top