WELEDI,USHUPAVU,UTII NA UNYENYEKEVU WAMPA SIMON SIRRO CHEO CHA IGP

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Joseph Magufuli jana amemteua Kamanda Simon Sirro wa kanda maalum ya Dar es salaam kuwa Mkuu wa jeshi la Polisi la Tanzania (Ispector General Police) IGP na kutengua uongozi ulikuwepo kwa Kamanda Ernest Mangu amabye alihudumu nafasi hiyo toka utwala wa awamu ya nne wa Jakaya Mrisho kikwete.

Simon srro atakuwa Kiongozi wa 10 kushika ktk nafasi hiyo ya IGP toka kuanzisha kwa jeshi la polisi,wengi wamezungumzia juu ya uteuzi huo na kuleta sababu nyingi kuhusiana na chaguo hilo.

Simon Sirro alishakuwa kamnda wa polisi kanda maalum mkoa wa mara amabpo kulikuwa na mauaji na fujo wa mara kawa mara hasa ktk wilaya za Rorya na Tarime ambako uhalifu wa unyanyasaji wa kijinsia,mapigano,wizi,imani za kishirikina,kilimo na bishara ya bangi,ukeketaji na ndoa za utotoni zilizokuwa zimeshamili kwa kasi kubwa,licha ya hayo yote kamnda Simon Sirro alijitahidi kudhibiti hali hiyon kwa kiasi kikubwa na kupunguza uhalifu huo ktk maeneo hayo.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa IGP na kuapishwa leo ikulu na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Simon sirro alikuwa kamanda wa kanda maalum wa jiji la Dar es salaam.














Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "WELEDI,USHUPAVU,UTII NA UNYENYEKEVU WAMPA SIMON SIRRO CHEO CHA IGP"

Back To Top