''HII NDIO TANZANIA YA VYOMBO VYA HABARI VYA KIDIJITALI"

Ziko sababu nyingi zinazoweza kufanya mtazamaji runinga kupata na kuona picha,video na sauti nzuri (HD OR 4K IMAGES) akiwa nyumbani kwake ametulia!

1.Moja ya sababu hizo ni aina ya taknologia,iliyotumika kuunda runinga anayoimiliki kama ya kisasa au zamani nikiwa na maana Flat tv (LED,LCD AU PLASMA) Au zile za kizamani maarufu za chogo!

2.Ni njia anayotumia kupata matangazo akiwa ni Analog au digitali.

3.Ni aina ya king'amuzi (decoder or receiver) kina ubora kiasi gani ktk kupokea na kutoa picha,video na sauti ktk ubora uliokusudiwa kama (MPG2,4,DVB,HD,4K).

4 Ni njia atakayotumia kuichukua matangazo hayo kutoka ktk kisimbuzi au king'amuzi chako kwenda ktk runinga yako ikiwa HDMI,DVB RF,VGA n.k

5.Ni aina ya satelaiti inayotumika kukuletea matangazo ktk king'amuzi chako kwa mfano Amos5,SSE 5,ASTRA,HOTBIRD n.k

6.Ni aina ya ya uunganishaji na vifaa vilivyotumika kukamilisha mzunguko kamili kuwa bora kufungwa na kufungwa kwa umakini wa hali ya juu,kwani makosa au matumizi ya vifaa duni yanaweza kufanya kupatikana kwa matangazo yaliyo chini ya kiwango.

7.Ni umakini na ujuzi wa fundi aliyetumika kuunganisha kuunganisha mtiririko mzima wa matangazo hayo,kwani makosa ktk kuelekeza dishi wanaweza kuleta matangazo hafifu na yenye kusumbua sana kwa mtazamaji bhusika kama kutika na kuganda kwa picha Mara kwa mara.

MSHANGAO WANGU NI HUU:-

Licha ya watu kujitahidi kuwa na runinga na vifaa vya kisasa kabisa bado baadhi ya vituo vya runinga nchini vimekuwa vikirusha matangazo duni sana ktk picha,video na sauti mbaya kabisa zisizovutia kwa mtazamaji.

Nimekuwa nikijiuliza shida iko wapi kwakuwa vituo hivyo vya runinga na redio vinavyotoa matangazo hayo duni cha kushangaza ni vinamilikiwa na serikali.

Usikivu na muonekano wake wa sauti,picha,video zake umekuwa wa hali ya chini sana kiasi cha kutomvutia mtazamaji wala msikilizaji.

Vituo vyetu vya taifa vya redio na runinga vimekuwa vikisika sehemu ndogo sana ktk nchi has a Mijini tu (Coverage) licha kuwa vyenyewe ndio vyankwaza kuanzisha kwa miaka zaidi ya 50 iliopita na kumilikiwa na serikali.

Urushaji wa matangazo wa vyombo vya habari vya serikali umekuwa duni na wa kusuasua na vipindi havipangili na wakati Fulani kushindwa kuweka matangazo ktk mda mwafaka hata ktk ya taarifa za habari.

Kinachonishangaza zaidi ni kuwa wataalam na wasomi Wengi waliobobea wako huko,mitambo bora,kisasa na imara zaidi iko huko lakini licha ya mambo yote hayo bado vituo hivi vimekuwa vikisuasua na kurusha matangazo chini ya ubora.

Nimekuwa nikijiuliza kwa mda mrefu sana! Hivi hawa wataalam,watangazaji na viongozi wa serikali huwa hawatazami aina ya matangazo wanayorusha wanapokuwa nyumbani kwao na wakaona udhaifu na tofauti na vituo vyengine vya ndani na nje

Nabaki kujiuliza tena tatizo ni wataalam,vifaa,mtaji na gharama za uendeshaji au usimamizi?

Kiukweli baadhi ya vyombo vya habari vya binafsi(redio na runinga) nchini mnakera sana watazamaji na wasikilizaji.

Ubovu na uduni huu wa matangazo kwa vyombo hivi ktk urushaji wa matangazo ktk vituo hivi utauona ktk kila baina ya kampuni aua kisimbuzi utakachotumia ukiwa ni Dstv,zuku,ting,azam,startimes,continental n.k

Sasa kwa ajili hiyo ya kila kampuni kituo hiko kuonekaa kinarush picha,sauti na video dunia hatuwezi kulaumu baina ya kisimbuzi au kampuni husika bali ni ubora hafifu unaotolewa na kituo husika.

Unapokaa kutazama vituo hivi inakubidi uwe na rimoti mkononi kwa ajili ya kupandisha na kupunguza sauti kwani ktk matangazo sauti huwa Kali sana na ya kustua na baadhi ya taarifa sauti huwa duni kiasi cha kutosikia wala kuelewa.

Hii inatia aibu sana kiasi cha kuona bora kipindi cha Analog matangazo yalikua bora kuliko sasa nyakati za kidijitali.

Wahusika walione hili na wakifanyie kazi haraka ikiwemo kuwekeza zaidi,kuandaa kipindi bora,redio kufika na kuwa na usikivu nzuri na masafa mrefu nchi nzima,kuwepo kwa mpangilio mzuri wa ratiba Maalum inayofuatwa na kuzingatiwa sio kukurupuka! Kuendesha vyombo vya habari ni gharama kubwa na lazima ukubali hivyo.

Yangu ni hayo tu!!!!!

juu ni runinga ya kisasa ya uso bapa na chini ni madishi makubwa yanayorusha matangazo yake kutoka ktk vituo au kupokea kkutoka ktk satelaiti

juu na chini ni studio za kisasa za vyombo vya habari za kimataifa zinazotumia vyombo vya kisasa kabisa ktk kutafuta,kutaarisha na kurusha matangazo yake


juu ni tv ya kisasa ikiwa inaonyesha picha angavu ya 4k ambayo huonyesha kitu kwa uhalisia wake na chini ni rimoti na king'amuzi cha kupokea matangazo toka ktk satelaiti.










juu ni dishi za majumbani kwa ajili ya kupokea matangazo kutoka ktk satelaiti na kuyapeleka ktk king'amuzi ili kuyatafsiri ktk video,picha na sauti.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "''HII NDIO TANZANIA YA VYOMBO VYA HABARI VYA KIDIJITALI""

Back To Top