ACHA MATUMIZI YA TUMBAKU NA UVUTAJI WA SIGARA KWANI UNAJICHIMBIA KABURI MWENYEWE HARAKA

Leo ni siku ya kuhamasisha kuacha kuvuta sigara duniani ikiwa na lengo la kupunguza au kuondoa kabisa matumizi ya tumbaku ambayo kwayo utumika kutengenezea bidhaahii hatari ya sigara za aina mbalimbali duniani.

China ndio nchi inayoongoza kwa watumiaji wa tumbaku duniani kote zikifutiwa na urusi,marekani,indonesia,japan,ujerumani,india,uturuki,korea kusini na vietnam kukiwa na watumiaji wa sigara wapatao bilioni 1ikiwa sawa na asilimia 20% ya watu wote duniani kote na hutumia zaidi ya sigara tilioni 5.8 ulimwenguni.

China,brazil,marekani,india,argentina,malawi na zimbabwe zikiwa ndio wazalishaji wakuu wa zao hili la tumbaku duniani,nchi hizi uzalisha zaidi ya tani milioni saba 7 kwa mwaka,wakiwa wanatumia hekta milioni 4.2 kulima zao hili.

Zaidi ya watu milioni 7 ufariki duniani kila mwaka kwa kutokan na matumizi ya tumbaku duniani.

Baadhi ya madhara yatokanayo na utumiaji wa tumbaku ni kama ya kupata kansa za koo,mapafu,kinywa,damu.

Kuharibu njia na miumo ya njia na mbegu za uzazi kwa wanawake na wanaume na kufanya kushindwa au kupata viumbe vilivyo na maumbile yasiyo sawa.

Kuharibika kwa mimba,kufa kwa kichanga kabla au baada ya kuzaliwa,kuzaa kabla ya wakati au watoto njiti,kuzaa watoto walio na uzito mdogo sana.

Kupata ugonjwa wa kifua kikuu aua Tb,maambukizi ya magojwa ya fizi,meno,pumu.

Kupata kulegea kwa viungo au kupalalaizi viuongo,kupata upofu,kupata shida ktk upumuaji,

Kuathiri utendaji kazi wa mifumo yote ya mwili kwa mvutaji na hata aliyekaribu na mvutaji wa tumbaku,kuleta harufu mbaya kinywani kwa mvutaji,kupasuka kwa mishipa ya damu.

Pia tumbaku ina sumu ya nikotini ambayo humfanya mtu kuwa mtumwa hivyo kuhisi uhitaji wa matumizi ya tumbaku wakati wote.

Tumbaku kifupi ina matatizo mengi kiafya na kimazingira hivyo ni muhimu sana kujiepusha na matumizi ya tumbaku kwa kulinda afya yako na wenzio ikiwemo na kulinda mazingira.

Tumbaku inaingiza pesa nyingi sana kwa wakulima na wafanyabiashara wa kati hata kwa serikali kupata mapato mengi kutokana na zao hilo hivyo kufanya kuwa ngumu kuacha kutokana na utajiri wa zao hilo.

Ila madhara yatokanayo na tumbaku ni makubwa zaidi ukilinganisha na faida zake.









Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "ACHA MATUMIZI YA TUMBAKU NA UVUTAJI WA SIGARA KWANI UNAJICHIMBIA KABURI MWENYEWE HARAKA"

Back To Top