Ule uhakiki uliofanywa kwa watumishi wa umma kwa baadhi ya idara toka mwezi oktoba 2016 ili kuhakiki uhalisia wa taarifa za wafanyakazi wa umma juu ya elimu zao walizopata ikiwemo na uwajibikaji na uwepo mahala pa kazi hatimaye umetimia jana baada ya waziri wa utumishi wa umma Angela Kairuki,kushirikiana na waziri wa Elimu Prof. Ndalichako kumkabidhi Rais John Pombe Joseph Magufuli Ripoti ya kazi hiyo ngumu Jana ktk ukumbi wa Chimwaga Dodoma.
Rais Magufuli aliipokea ripoti hiyo ndefu iliyoandaliwa ktk mtindo wa vitabu kadhaa mbele ya wageni na wanachuo wa UDOM akiwa na Makamu wa Rais Samia suluhu hassan,waziri mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.
Rais Magufuli alisisitiza kuwa serikali imeibiwa vya kutosha na aina hii ya udanganyifu wa wahuni wachache na mawaziri wa serikali zilizopita wakiwa kimya kana kwamba hawaoni au hawajui kitu hiki,Rais alisisitiza kuwa wafanyakazi hawa 9,932 kufikia mwezi mei 15 wanatakiwa wanatakiwa kutoka ktk maeneo ya kazi na kuacha nafasi hizo wazi kwani Serikali imeshatangaza maombi mapya ya ajira 64000 watu waombe, Na wale watakao kaidi kutoka mpaka mkono wa sheria uwafikie basi watakamatwa na kufunguliwa kesi hatimaye kufungwa kifungo cha miaka 7 jela kwa makosa ya kutumia nyaraka hizo za vyeti bandia au vya kughushib kuomba kazi na kutunia mali za umma pasipo halali.
Uhakiki huu wa vyeti vya wafanyakazi wa umma haujahusisha baadhi ya wafanyakazi wa umma kama wabunge,mawaziri,wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya na ngazi zote a kuteuliwa ambazo msingiwa kazi zao wanahitajika kuwa na sifa za kujua kusoma na kuandika tu.

0 Comments "WATUMISHI WA UMMA 9,932 KUFUNGIWA MISHAHARA MWEZI MEI KWA MATUMIZI YA VYETI BANDIA"