Ndege huyu mwenye uzito wa kilo 4 hadi 6.5 na urefu mbawa futi 7.5 zinazomwezesha kupaaa kwa haraka na kuweza kunyanyua vitu vizito kama mbuzi,sungura,samaki na hata nyoka wakubwa.
Chakula kikuu kwa ndege huyu ni Nyama na wadudu mbalimbali ambao ukamata kwa kutumia,mdomo na miguu yake mikubwa,imara na yenye kucha Kali sana za kuweza kutoboa na kushika kiumbe bila kuanguka
Tai macho yake yenye uwezo mkubwa wa kuona mara 8 zaidi ya mwanadamu ktk kuona vitu umbali kilomita tatu (3.2) sawa na mita 3200 kutoka aliko yeye akiwa angani.
Tai wa kike wanakuwa na maumbile na uzito mkubwa zaidi kuliko wa kiume, tai utaga mayai matatu na kuyatunza kwa Siku 35 hadi kuyaangua.
Ni mara chache sana kwa ndege huyu kuona kitu au mnyama kuwinda na kukosa au kukamatwa yeye kwani macho yake yanaona sana na ana nguvu nyingi za kukwapua kitu akitokea angani kwa spidi Kali sana na kuichukua alichokusudia ikiwa msituni,juu au chini ya maji na hata ktk milima na miti mirefu.
Tai uishi kwa miaka baina ya 20 na 30.
0 Comments "MJUE NDEGE HUYU TAI (EAGLE) MLA NYAMA MWENYE NGUVU ZAIDI."